REDEMPTION(KULIPIWA DENI/WOKOVU)
Kuna
maneno Mawili ya kingereza yanayoweza
kutumika kwaajili ya kuelezea Neno Ukombozi,maneno haya ni Deliverance na
Redemtion.Maneno haya mawili ni maneno tofauti sana lakini yanayofanya kazi
pamoja,na kutokana na namna ambavyo yanamaana karibia sawa za utendaji kazi
wake,si watu wengi wanaweza kutofautisha.
Tunaposema
Redemtion ni neno linalotokana na Tendo redeem, ambapo tafsiri yake ni
kukombolewa kutokana na Deni ulilokuwa unadaiwa, mfano tunaposema huyu amekuwa
redeemed, tunamaana hapo kwanza aliwekwa rehani kwa sababu ya Deni alilokuwa
akidaiwa.
Katika
maandiko Neno hili linamaana ya moja kwa Moja juu ya wokovu wetu,tunasoma
Galatia
3:13
Kristo
alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu;
maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
katika andiko hilo hapo juu utaona neno ukombozi
katika biblia ya kingereza ni redeemed,na sio delivered, hii ni kwa sababu
ukombozi kwa maana ya andiko hapo juu ni kulipiwa deni.
kwa namna rahisi tunaweza tukasema hivi “Kristo alitulipia deni la torati,kwa kuwa
alifanywa laana kwaajii yetu/niaba yetu”
kwa hiyo Yesu alilipa deni tuliyokuwa tunadaiwa ili tuweze kuwa wa
kwake yeye,na hii ndio tafsiri hasa ya ukombozi kwa mlengo wa wokovu.
Lakini pia tunaposema hasa juu ya wokovu
tunazungumzia juu ya kufanywa upya juu ya roho ya mtu, tunasoma 2cor 5:17
Mtu akiwa ndaniya kristo amekuwa kiumbe kipya,maneno
haya yanamaana kubwa sana ya wokovu,neon mtu tunafahamu kuwa huzungumzia roho
ya mtu na sio nafsi wala mwili kwa sababu mtu mwenyewe ni roho na anaposema
ndani ya kristo ni sawa na kusema ndani ya Roho mtakatifu anafanyika kuwa
kiumbe kipya ya kale yaani ule utu wa kale ambao ulikuwa ndani ya mauti na
dhambi unafanywa upya kwa kule kuwa ndani ya Roho Mtakatifu,na huu ndio ubatizo
wa Roho mtakatifu(Rejea kitabu cha Viwango vya Roho Mtakatifu).
Sasa kumbuka mtu si roho pekee,bali anayo nyumba
inayoitwa mwili na iliyopewa nafsi(akili,utashi na moyo) na kwa sababu hiyo
unaposhughulikia oho yako kwa kuupokea wokovu ni lazima pia utiishe mwili wako
ili kufanya mapenzi ya MUNGU,hii ni kwa sababu mwili kwaasili hauwezi kuokoka
biblia inasema
(mwili ni wa mauti)
Asili ya mwili ni chini na ni mauti wakati roho yako
asili yake ni ya juu.katika kuutiisha mwili ni Pamoja na kuvifisha viungo na
kufungua vifungo vilivyofunga nafsi yako na mwili wako ili mwili na nafsi yako
isiwe kikwazo kwa roho yako katika kutenda mapenzi ya Mungu. Hii ndio sababu
utaona Biblia inasema mwili unapokuwa na Nguvu hupingana na roho yako na
kwasababu hiyo hutaweza kufanya mapenzi ya Mungu kikamilifu.
Galatia 5
Mfano: jaribu kufikiri unaweza ukawa unatamani sana
kwenda kanisani na umeamka asubuhi unakuta mwili wako ni mgonjwa wote,je
utakwenda? Au unajua wapo watu ambao wanatamani sana kuomba lakini kila
wakijaribu kuomba wanasikia uchovu gafla na wanajikuta wanakosa hamui ya
kufanya maombi,Je unadhani hiyo ni hali ya kawaida? Ni vifungo vilivyoko katika
mwili ambavyo visiposhughulikiwa vinazuia roho yako kufanya mapenzi ya MUNGU.
Na hapo ndipo inapohitajika kufanya ukombozi yaani deliverance ili kupokea
uhuru kamili.
DELIVERANCE
Tunapozungumza juu ya deliverance hatugusi juu ya
kazi ya Yesu ya msalaba kwa maana ya kulipiwa deni (redemption) kwa kuwa
deliverance ni tendo linalofuata baada ya redemption. Na kama tulivyotangulia
kuangalia hapo mwanzoni kuwa ni roho ndio hupokea wokovu,kwa namna nyingine
naweza kukwambia kuwa roho yako haiitajio deliverance inahitaji redempition kwa
sababu unapompokea Yesu kristo Yeye mwenyewe kwa damu yake anatufanya kuwa
wapya katika roho. Kinachotokea baada ya kufanywa upya kwa roho yako unahitaji
kuanza kushughulikia vifungo vilivyoko ndani ya nafsi na mwili wako ili kuleta
wepesi wa roho yako kufanya mapenzi ya Mungu. Ili kuelewa zaidi tuangalie mfano
huu uliopo ndani ya Neno la MUNGU.
yohana
11:43
Naye
akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44Akatoka
nje yule aliyekufa, akiwa amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake
amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
kwa Mfano huu tunaweza kuelewa uhusiano kati ya
ukombozi(redemption) na ukombozi(deliverance)
katika maandiko yaliyopo hapo juu utaona matukio
yaliyotokea na kufuatana katika kumfufua lazalo na nitajaribu kuainisha kila
kipengere cha tukio ili uweze kuelewa zaidi.
a. Liondoeni
Jiwe
Lazaro
ni mfano wa mtu aliyekatika dhambi,ambaye hajaokoka wala hamjui yesu,mtu wa
aina hii maandiko yanaweka wazi ya kwamba anajina la kuwa hai lakini anakuwa
amekufa roho yake(ametengwa na Mungu)
ufunuo
3:1
Na
kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na
hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una
jina la kuwa hai, nawe umekufa.
sasa mtu huyu roho yake inapotengana na Mungu mapepo
huweka kifuniko juu yake ambalo ni mfano wa jiwe katika kaburi la Lazaro ili
kusudi asisikie injili ya kristo asije akafufuka na hata akifufuka ashindwe
kutoka nje.
Hiii ndio sababu
Yesu anaagiza “liondoeni jiwe” maana yake fanyeni maombi
yatakayotengeneza mazingira ya kifuniko juu ya watu wenye dhambi kuondolewa. Ikumbukwe
kuwa Mungu hafanyi kitu duniani isipokuwa mtu mmoja ametengeneza nguvu ndani
yake ili azitumie kufanya mambo makubwa,na nguvu hii hutengenezwa kwa njia ya
maombi.
kwa hiyo kama watu wasipoomba juu ya eneo wanalotaka
watu waokoke,wanaweza kushangaa wanahubiri sana na watu hawaokoki au wanaokoka
lakini wanarudi dhambini, hii ni kwasababu wanakuwa na kifuniko bado juu ya
maisha yao.
b. Yesu
akamwita lazaro Toka nje
Sasa
hii ni hatua ya pili baada ya kuondoa jiwe Yesu anamwita lazaro (mwenye dhambi)
aje katika wokovu, tukumbuke kuwa anayeokoa ni Yesu kristo na si mwanamaombi.
sasa katika hatua hii Yesu anamwita lazaro atoke nje,awe hai, na lazaro
anatoka,huu ni mfano wa ukombozi kwa maana ya redemption.
c. Mfungueni
sanda mkamwache aende zake
katika
hatua hii Yesu anaagiza Yule aliyetoka kaburini na sanda afunguliwe sanda ili
awe huru kabisa,huu ni mfano wa ukombozi kwa maanda ya deliverance,ya kwamba
mtu anaweza akawa ameokoka (amefufuka) na ametoka kaburini lakini bado yuko
chini ya vifungo (sanda) vitakavyomfanya pamoja na kuwa amepokea uzima wa
milele ndani yake,kuna vifungo katika mwili wake na nafsi yake vinaweza
vikamfanya akapoteza uzima wake.
Redemtion
hushughurika na roho yako na deliverance hushughulika na mwili wako.
1cor 5:7
Basi,
jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile
mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka,
yaani, Kristo;
unaweza ukawa umeokoka lakini kwa sababu ya chachu
ndogo katika mwili wako ukashindwa kuuona wema wa Mungu katika maisha yako.
hivyo basi Deliverance ni jumla ya maombi
yanayomfungua Mtu kutoka katika sanda au chachu ili afurahie uhuru wake ndani
ya Kristo Yesu
Kitabu hiki kipo kwaajili ya kukusaidia kuiona
chachu na sanda mbalimbali katika vipengera tofauti ili uweze kuomba na
hatimaye kufunguliwa kabisa vifungo,unaposoma kitabu hiki ni maombi yangu
kuwa Roho wa Mungu akuwezeshe kuona
zaidi ya kile kilichomo ndani ya kitabu hiki ili uweze kupokea uhuru kamili
katika Jina la Yesu.
MAELEZO
MUHIMU
Ndani ya kitabu hiki utakuta vipengere
mbalimbali vinavyoelezea aina ya jambo linalohitaji kufunguliwa pamoja na
Maelekezo ya namna ya Kuweza kuomba.
hivyo basi Fuata maelekezo hayo kwa
usahihi ili kuweza kupoke kile unachoomba,kama nyumbani kwako hauna mafuta ya
ukombozi/unaweza ukayapata kwa kuja kanisani au ukatumia mafuta yoyote ambayo
umekwisha kuyaombea kama kipitishaji cha upako wa Roho Mtakatifu(Channel of
Anointing).
MAOMBI
YA UKOMBOZI
1.
KATAA
KUWA SEHEMU YA MAISHA YALIYOPITA
kuna watu wengi wanaishi maisha ambayo
siyo ya kwao,na wanajaribu kujinasua na kutoka katia maisha hayo lakini kwao
inakuwa sio rahisi,kulingana na hali waliyonayo na mazingira yanayowazunguka
kila siku. Wewe unaweza ukawa ni mmoja kati ya watu wa namna hiyo, ambao watakalo
kulifanya hawafanyi lakini wanafanya wasilo litaka.
warumi 7:15
“Maana
sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo
ndilo ninalolitenda”
Usijilaumu juu ya kile unachokipitia,kwa
sababu inawezekana si makosa yako mpaka umefika hapo,labda unaweza ukawa unapitia
kile kile ambacho Mtume Paulo anakizungumza katika mistari hiyo tuliyoipitia,au
labda wewe ni matokeo yanayofanana na hali ya mafarisayo wakati wa Yesu
mathayo 23:29
Ole wenu, Waandishi na
Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba
maziara ya wenye haki, na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu,
hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya
kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.
Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya Jehanamu? Kwa sababu hiyo,
angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine
wao ninyi mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi
yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; hivyo ije juu yenu damu yote ya haki
iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya
Zakaria mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.
kitu kimoja ambacho si watu wengi
wanakijua ni kuwa,sheria ya uumbaji inafanya kila kitu kuzaa kitu kinachofanana
nacho yaani kila kitu hujizidisha katika namna ile ile ambayo iliumbwa tangia
mwanzo
mwanzo 1:29
“Mungu
akasema, Tazama, nimewapa kila mmea utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote
pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa chakula chenu”
mfano ni kama hilo andiko hapo juu,unaona Mungu
anaumba Matunda ambayo ndani yake yanambegu za kuzalisha matunda ya aina ileile
ambayo imetoka,mchungwa kuzaa mchungwa,mpera huzaa mpera,mtu huzaa Mtu,na
mnyama huzaa aina ileile ya mnyama,hiyo ndio sheria(order) ya uumbaji.
Kwa kule kusema aina ilele ya uumbaji ninamaana kila
mbegu ndani yake hubeba vinasaba(genes) ambavyo ndani yake vimebeba tabia,na
alama za ukoo.
mwanzo 49:3
Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,
Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo
wangu.
Umewapita wengine kwa ukuu na kwa
nguvu.
unaona reubeni kama mzaliwa wa kwanza
amebeba nguvu ama uwezo wa yakobo na kama yakobo alivyowapita wengine vile vile
na reubeni. sasa ukiangalia mistari ile ya mathayo 23,utaona ile oda ya uumbaji
ikiendelea kwa mafarisayo.
pamoja na kuwa mafarisayo hawakupenda
yale ambayo baba zao waliyafanya,hawakuwa na namna ya kujiepusha nayo kwa
sababu yalikuwa ndani ya damu yao na walikuwa tayari wameanza kuyafanya bila
kujua,Baba zao waliwauwa manabii na wenye haki huku watakatifu wengine
wakiwafukuza mji kwa mji,na hapa bila kujua walikuwa wakipanga njama za kumuuwa
Yesu,hiyo ilikuwa katika damu zao na isingeweza kuepukika kirahisi,kwa sababu
wao walikuwa ni malimbuko na uwezo wa wazazi wao.
wakati mwengine unaweza ukajikuta kile
ambacho ndani ya roho yako unatamani sicho unachokifanya,unajikuta unapitia
yale yale ambayo baba zako waliyapitia,inawezekana unapitia umasikini ule ule ambao
baba zako waliupitia,magonjwa yale yale ambayo baba zako waliumwa,na shida zile
zile.kama walizo pitia wazazi wako. hiyo inaitwa laana ya vizazi (generation
curse)
lakini habari njema ni hii siku
ulipookoka Mungu aalikupandikiza katika ukoo wa ibrahimu,isaka na Israel wagalatia 3:14,hivyo unapokea haki kwa
hiyari yako kujinasua katika laana ambayo ilikuwa juu ya wazazi wako,mababu
zako na wahenga wako wote,unahaki ya kuchagua kuishi maisha yako na si maisha
yao.
pamoja na kuwa wewe hukupanga uwe kama ulivyo,na
hali hiyo inakusumbua na unatamani kuachana nayo lakini unashindwa,hii ni
kwasababu wewe umebeba aina ile ile ya wazazi (genes) na hivyo ili uweze kutoka
katika uharibifu huo unahitaji aina nyingine ya vinasaba,Tunasoma
Galatia
3:13-14
“Kristo alitukomboa
katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana
imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14ili kwamba baraka ya Abrahamu
iwafikie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya
imani”
Laana ya torati ni laana ya sheria,ni matokeo ya
sheria inapovunjwa au kuharibiwa au kutofuatwa,sasa kama sheria ya uumbaji
ilitaka watu wafanane na Mungu mwanzo 1:26,lakini wakachagua kuvunja sheria na
kutaka kufanana na adui,laana ambayo ni kisasi cha sheria huingia kwenye mifumo
yao.
labda nijaribu namna hii,ikiwa neno la Mungu ndio
sheria Njema ya uumbaji,na sheria hii ilisema,Na tumfanye Mtu kwa sura(roho) na
mfano(nafsi) wetu mwanzo 1:26,maana yake lile neno jema yaani sheria lilikaa
nda ni ya nafsi ya Mtu na roho ya Mtu na kuleta mtiririko wa vinasaba vya
kiungu (genes) katika nafsi na roho ya Mtu na kumfanya awe nafsi hai,ni hivyo
kufanya kila kilichozaliwa kwa Yule mtu wa kwanza kuwa na aina ya uungu na
uhai.
halafu kisha Yule mtu aliyepokea ile sheria ya uzima
akaamua kusikia neno la Mauti kutoka kwa shetani kwa hiari yake,maana yake ni
kuwa alichagua mtiririko mwingine wa vinasaba ndani ya nafsi yake na roho yake
ambavyo,badala ya kuleta Uzima ndani yake vilileta mauti na japokuwa mtu
alibaki na sura na mfano wa Mungu mtiririko wa uhai ulibadilishwa na kuwa
mauti,na kulingana na sheria ya uumbaji kama tulivyoona mwanzo 1:29,kila mtu
aliipokea mauti hata kama hakutaka.ona.
warumi
5:12
Kwa
hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti;
na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi
hivyo inapotokea babu zako baada ya
adamu waliingia katika mikataba mbalimbali ya kishetani kama
matambiko,uganga,uchawi ili kupata msaada wa kipepo,au walimwaga damu ya mtu
asiye na hatia ili kupata mali kwa nguvu au kulipiza kisasi,waliaribu pia
mtiririko wa vinasaba vya uumbaji,kwa hiyo hata kama haukutaka kuwa hivyo
utakuwa kwa sababu ya kilichopo ndani ya Damu yako
lakini Habari njema ni Kuwa kifo cha
yesu kilivunja hiyo sheria na
kutuunganisha na mtiririko ulio bora zaidi,ya ule wa kwanza kwa hiyari yetu.
unapokubali na kumwamiini Yesu Kristo,unahamishwa kutoka katika mtiririko wa
mauti na kuingia katika mtiririko wa uzima,na kuanzia kwako kila utakacho zaa
kitakuwa na uzima.
NAMNA YA KUVUNJA MTIRIRIKO NA VINASABA
VYA MABABU ZAKO NA KUPOKEA VINASABA VIPYA KATIKA MAISHA YAKO.(DELIVERANCE FROM
GENERATION CURSE)
1. NI
LAZIMA UOKOKE
Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa
sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi ili kwamba, kama vile
dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale
hata uzima wa milele kwa Yesu
Kuokoka ni hatua ya kwanza inayokufungua kutoka
katika vifungo vya dhambi ya Adamu,na kukupa haki na neema ya kutoka katika
vifungo vingine kwa hiyari yako mwenyewe.
ili kuuona ufalme wa Mungu(yaani kuwa na utawala wa
Mungu katika maisha yako) kuzaliwa mara ya pili(kuokoka) ni lazima.
Yohana
3:3
Yesu
akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili,
hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
2. OMBA MAOMBI YA KUJITENGA NA LAANA ZA VIZAZI
ikiwa Babu zako au wewe mwenyewe
uliingia katika mikataba ya kishetani ili kupata msaada,ili kutoka utahitaji
wewe mwenyewe kujitoa kupitia damu ya Yesu. Damu ya yesu ipo kwaajili ya
kukusaidia utoke katika hiyo mikataba ya kipepo utakapoamua kutoka.
ufunuo 12:11
“Nao
wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao
hawakupenda maisha yao hata kufa”
mwisho wa somo hili utaona kuna maombi ya ukombozi(prayer
point) anza kuomba hizo na utaona Mungu akikufungua na kukuweka huru,bila shaka
pia unaweza ukahudhuria katika ibada zetu za maombi ya ukombozi kila alhamisi
na Jumapili katika Makanisa yetu ya URU(ubalozi wa Roho wa Uzima) Ministries
3. KULA
MWILI NA DAMU YA YESU
Mwili na Damu ya Yesu ni siraha lakini
pia ni vifaa vya kiungu kwaajili ya kukupandikiza katika uzao wa kiungu
yohana 6:56
Aulaye
mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57Kama
vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye
mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. 58Hiki
ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa;
bali akilaye chakula hicho ataishi milele
Mwili wa Yesu katika umbo la Mkate na Damu ya Yesu
katika umbo la Divai hufanya mtu kuunganishwa katika uzao na mtiririko wa
vinasaba vya kiungu na hivyo kupokea uhai kutoka kwa Mungu, Yesu anasema mababa walikula chakula ambacho si mwili na
damu ya Yesu nao wakafa au kwa tafsiri nyingine wakaleta mauti,Yeye atakaye mla
yeye atapokea tena mtiririko wa uzima ndani yake.
unapokula mwili wa Yesu unapokea Baraka zitokanazo
na kazi ya Yesu ya msalaba ambazo ni uponyaji kutoka katika magonjwa ya aina
zote, isaya 53:5, unafunguliwa kutoka katika umasikini wote 2corth 8:9 na pia
unapokea kuhuishwa upya.
unapokunywa damu ya Yesu unaingiza vinasaba(genes)
ndani ya nafsi yako na Damu yako na hivyo kupokea Mbegu na aina ya mbinguni,na
kama kuna agano lolote huvunjwa kwa hiyo damu ya Yesu. kwa kule kunywa Damu ya
Yesu kila magonjwa ndani ya damu na nafsi huharibiwa kabisa.
4. SOMA
NENO LA MUNGU NA KULIISHI
Neno la Mungu huleta virutubisho vya
uzima ulioupokea na kwa kadili unavyozidi kusoma na kuishi ndani ya Neno, Ule
utu upya ulioupokea huuwishwa kila siku na kukua hata kufikia mtu mkamilifu.
Yohana
1:1-5
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye
Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa
Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; nwala pasipo yeye hakikufanyika chochote
kilichofanyika.Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya
watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
.
MAOMBI YA UKOMBOZI
1. Baba
katika jina la Yesu ninatubu kwa makosa na dhambi na uovu uliofanywa na wahenga
wangu ambao umeletwa juu yangu na uzao wangu,ninamwaga Damu ya yesu katika
malango ya kuzaliwa kwangu na ndani yangu katika jina la Yesu
2. Ninajitenga
na kila laana za mababu na mabibi zilizoko juu ya maisha yangu,ninakata kila
mti wa laana za kurithi kutoka kwa mababu na mabibi,na ninajipandikiza katika
uzao wa Yesu kriso ambao ni uzao wa Ibrahimu.
3. Ninarudisha mamlaka yote aliyopewa
shetani na mababu/mababa ,katika Jina la Yesu.
4. Nina zilaani roho zote zinazoendelea
kutilia mkazo hayo maagano katika maisha yangu na naziamuru kuniachia kwa Jina
la Yesu[ Sema mara 3 na anza kusema hivi,”niachie kwa jina la Yesu
5. kila
roho simamizi zinazo zidi kutilia mkazo umiliki wake juu yangu ziteketee kwa
Moto wa Roho mtakatifu katika Jina la Yesu Kristo.
6. ninatangaza
kuwa mimi si sehemu ya uovu wao,Damu yao,Laana zao. mimi ni mzao wa
Ibrahimu,ukuhani wa Kifalme taifa takatifu tu wa milki ya Mungu.
maelekezo ya kinabii:
Chukua
mwili na Damu ya Yesu kisha kula na Kunywa,kisha tangaza uhuru wako kutoka
katika laana ya Vizazi
KUFUNGULIWA
NIRA
Kwa wale walioko
vijijini au umewahi kuona maisha ya mashambani huko vijijini unaweza ukaelewa
pale biblia inapozungumza juu ya Nira.
nira ni kifaa
kilichotengenezwa kwa Miti na miti hii hufungwa shingoni mwa ngombe,lengo hasa
ni ili kumsaidia mkulima kuwaongoza ng’ombe vema wakati wa kulima,nira
inapofungwa juu ya ng’ombe au punda,unaweza kumwongoza mahali popote
unapohitaji aende,utambebesha mizigo na kumwongoza apeleke mahali popote.
katika
ulimwengu wa roho kuna mfumo unaofanana na huo katika ulimwengu wa giza,mapepo
yanapotaka kumwongoza mtu mahali yanapotaka humfunga kwanza huyo mtu ndani ya
nira,na kisha humtwisha mizigo na kumpeleka mahali popote yanapohitaji aende.tofauti
yake huwa nira hizi huwa sio miti isipokuwa aina Fulani ya roho,zinapandikizwa
katika maisha yako ili kukufanya ufanye vitu bila wewe kutaka.
Mfano
mzuri wa roho hizi ni Roho za madeni,ulevi,uzinzi n.k
kwa
kupandikiza roho hizi mtu hatakuwa na maamuzi juu ya mapato yake anayoyapata na
maisha yake,hii ndio sababu unaweza ukakuta mtu anapata fedha halafu yote
inaishia baa,inaishia kwenye madeni,au kulipia bili za hispitali.
Chini
ya roho hizi mtu hataweza kufanya maendeleo yeyote,mtume na Nabii Paulo anasema
warumi
7:15
Sielewi
nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda
lile ninalolichukia
unaweza
ukawa hupendi kwa hakika kile unachokifanya,lakini unajikuta unafanya hata kama
hupendi,unajaribu kuacha lakini badala ya kuacha unajikuta ndio kwanza
umechochea,ni kwa sababu umefungwa nira na hautaweza kutoka hapo mpaka Yesu
Kristo akufungue.
mara
nyingi roho hizi huingia ndani ya mtu
pale Mtu anapofungua mlango wa haya mapepo kuingia,kwa faida nitakwenda
kukuonesha milango hiyo ya kipepo ili usiwe muhanga tena wa kuvikwa nira.
1.
Dhambi
huu
ni mlango mkubwa wa Mapepo kuingia ndani ya Mtu,maandiko yanasema
1yohana
3:8
Yatendaye
dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi
hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
2. Kupitia
kupokea au kuona vitu vilivyolaaniwa(cursed materials)
huu ni mlango wa pili
wa ambao shetani huutumia ili kuingiza roho za uharibifu katika maisha yako,kila
kitu kinachoonekana kina uwezo wa kubeba roho kwa sababu kina mwili,na kwa
sababu hiyo ni rahisi kwa vitu kuweza kutumiwa na shetani katika kubeba roho
zitakazo haribu maisha yako,sio watu wengi wanajua ya kwamba hata tu kwa kule
kuona vitu vilivyobeba roho unaweza kupokea hiyo roho chafu
ayubu 31
Nilifanya
agano na macho yangu;
Basi
ningewezaje kumwangalia msichana?
macho ni
mlango wa moyo na mwili,kwa sababu kwa kuona mtu hupokea imani na imani
ni
roho,hivyo hivyo kupitia kuona unaweza ukapokea roho za uasherati,ulevi,uasi
n.k
dawa ya kutokuvamiwa
na roho zinazowinda macho yako ni kupitia kuweka agano na macho yako lakini pia,hii
ndio sababu unaona mtume Paulo anasisitiza juu ya kutakasa vitu kwa neno na
kuomba.
1timotheo 4:5
“kwa
kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”
Angalia
mstari huu
zaburi
119:91
Kwa hukumu zako vimesimama imara
hata leo,
Maana
vitu vyote ni watumishi wako.
kwa kule kusema vitu
vyote ni watumishi wako,ina maana vitu vinaweza kutumika katika kutekeleza
makusudi Fulani,unapokomboa kitu chochote kwa maombi na kwa neno unaviweka kuwa
chini ya Mungu kwaajili ya Utumishi,lakini usipovikomboa vinaweza kutumika na
shetani ili kubeba roho za uharibifu na hivyo kukufunga katika maisha
yako.fikiria kama magari yangekuwa watumishi wa Mungu ajali zingetoka wapi!.
3. Ndoto.
Ndoto pia ni mlango wa
adui,hasa inapotokea mtu amelala bila kuwa na ulinzi wa Mungu,unapoomba wakati
wa kulala unaruhusu Mungu kutawala mipaka na malango ya roho yako na nafsi yako
na hivyo kumfanya shetani kukosa mlango wa kuingia na kuharibu.
matayo 13:25
“lakini
watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda
zake”
unaona
watu walinapolala bila ulinzi wa Mungu shetani huja na kupandikiza roho za
uharibifu ndani ya maisha yao kwa njia ya ndoto,mfano wa ndoto ambazo
hudhihirisha uvamizi wa adui ni kama mtu anapoota anakula vyakula hasa nyama
asizozijua,kuota unakimbizwa na nyoka,kuota unafanya tendo la ndoa na mtu
unayemfahamu au usiyemfahamu n.k
hii
ndio sababu imeandikwa
zaburi 127:1
BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wanafanya kazi bure.
BWANA
asipoulinda mji
Yeye
aulindaye anakesha bure.
hakikisha unapoamua kulala,unapata muda wa
kuomba na kutafakari neno la Mungu.
kama
umekuwa muhanga wa maeneo hayo na hata ambayo sijayataja usiogope,habari njema
nikuwa
isaya 10:27
Tena
itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake
shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.
siku
ya leo nisiku ambayo kila nira juu ya maisha yako inakwenda kuvunjwa,na kila
mzigo(majukumu) ambayo shetani amekutwisha mabegani mwako yataharibiwa kwa damu
ya Yesu.
Mungu
anakwenda kuku weka huru Muda Mfupi ujao,utakapoamua kufuata maombi haya ya
kinabii,hii imehakikisha.
maelekezo ya kinabii:
Chukua mafuta ya
Ukmbozi (oil of Deliverance) kisha paka
kichwani kwako na shingoni mwako kisha anza kuomba maombi haya.
1. Baba
katika jina la Yesu kila nira ambayo shetani ameiweka katika maisha
yangu,iharibiwe sasa kwa mafuta haya.
2. kila
mzigo wa majukumu ambao shetani amenitwishwa ili kunifanya masikini,mnyonge na
dhaifu ninauondoa sasa katika jina la Yesu.
3. kila
wachungaji wa kipepo wanaolazimisha bado nia kubaki kwenye maisha yangu
waharibiwe kabisa na kuwa majivu katika jina la Yesu
4. ninatangaza
uhuru wangu,kutoka katika katika kila nira za magonjwa,umasikini,madeni
n.k(taja)
5. ninatangaza
kuwa mimi ni mwali wa Moto na hakuna silaha itakayofanyika juu yangu
itafanikiwa katika jina la Yesu Kristo.
3.
KUSHUGHULIKIA ROHO YA HOFU YA KIPEPO.
kuna
aina mbili za hofu ambazo zimatajwa katika biblia
1. hofu
ya Mungu
2. Hofu
ya kipepo
HOFU YA MUNGU
hofu
ya Mungu,biblia inasema ndio uchaji,yaani kumcha Mungu na kuchukia uovu,ni
kutetemeka unaposikia neno la Mungu,isaya 66:2
hofu
ya aina hii huletwa na Roho mtakatifu na ni moja kati ya roho saba za Mungu
zilizoachiliwa kwa watoto wa Mungu isaya 11.
HOFU YA KIPEPO
aina
ya pili ya hofu ndiyo nataka twende tukaishughulikie siku ya leo,ni hofu ya
kishetani au hofu ya kipepo,Aina hii ya hofu ndio mlango Mkubwa wa shetani
anapotaka kuharibu maisha yako,mara nyingi kabla shetani hajaharibu maisha ya
mtu,hutafuta mlango wa kuingia katika eneo la Maisha yako,na moja kati ya vitu
ambavyo anatumia ni vitisho vinavyotengeneza mlango wa hofu, na kisha
akishapata mlango huingia ndani na kufanya uharibifu.
hii
ndio sababu utaona katika neno la Mungu,mara nyingi Mungu anapotuma malaika au
Yesu kristo anapowatokea wanafunzi wake huanza na neno “Usiogope” kwa sababu
ukiogopa mlango wa mapepo hufunguliwa na hivyo kumzuia Mungu kufanya kazi.
dada
yangu na kaka yangu,hofu ni roho inayotoka kuzimu,haitokani na Mungu,hofu ya
aina yoyote,hofu ya usiku yaani huwezi kulala peke yako,bila taa,huwezi kupita
makaburini,hofu ya wachawi,hofu ya magonjwa,hofu ya umasikini,hofu juu ya mambo
ya baadae,hofu ya talaka,hofu ya kushindwa,zote na nyinginezo,hazitokani na
Mungu,ndio maana maandiko yanasema
2timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa
roho ya woga,(hofu) bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
unaporuhusu
roho ya hofu tu ndani yako ndipo uharibifu hutokea,roho ya hofu huzuia uwepo wa
Mungu katika maisha yako
waebrania 10:38
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.
pindi tu unapookoka unaitwa mwenye
haki wa Mungu,na mategemeo ya Baba Mungu ni kuwa uishi maisha ya imani kinyume
na hofu,mwenye haki anapoanza kuruhusu hofu za kipepo katika maisha yake
humfanya Mungu kuhuzunika na kutokuwa na furaha naye.
siku
ya Leo ninakemea roho ya hofu ndani yako ikuache mara moja katika Jina la Yesu
kristo,karibu sasa tuanze kuomba.
maelekezo ya kinabii:
Chukua mafuta ya ukombozi,na kisha Jipake katika kichwa chako na uombe maombi
haya.
Maombi.
1. katika
Jina la Yesu Kristo,ninaharibu kila milango ya hofu katika Maisha yangu kwa
damu ya thamani ya Yesu Kristo
2. Ninag’oa
kila mapando na visababishi vya roho ya hofu katika maisha yangu Katika Jina la
Yesu
3. ninakataa
kuwa mtumwa wa Hofu na mashaka ya aina yoyote,hofu ya usiku,hofu ya
kifedha(taja aina ya hofu inayokusumbua) katika jina la Yesu.
4. roho
mtakatifu,Nipatie roho ya Nguvu na ya moyo wa Kiasi katika Jina la Yesu
UKOMBOZI WA MIGUU
Ni muhimu sana kufanya ukombozi wa Miguu
mara kwa mara hii ni kwasababu ya umuhimu wa miguu katika mafanikio ya Mtu
binafsi na hata maeneo husika.Katika maandiko Miguu ni eneo linaloanzia katika
maungio ya kiuno mpaka chini kabisa ya nyayo za Mtu, eneo hili hasa nyayo ni
maeneo Muhimu sana ya kuyaangalia unapofanya Maombi ya Ukombozi, sasa hebu
tuangalie Jinsi gani Miguu inaumuhimu katika umiliki wa maisha ya Mtu
1.
Miguu
ni malango ya kumiliki
Yoshua
1:3-4
Angalia mahali mtakapokanyaga miguu yenu
nimewapa,kwa tafsiri nyingine Mungu anajaribu kusema ninatumia nyayo zenu
kupitisha umiliki katika maisha yenu.
hii ndio sababu ni muhimu sana kulinda
mahali nyayo zako zinakanyaga kwa sababu mahali utakapokanyaga
utapamiliki,unaweza usimiliki katika ulimwengu wa mwili lakini katika ulimwengu
wa roho unapokanyaga mahali kama mtu wa Mungu nyayo zako zanaanza kumiliki kila
kilichopo katika hilo eneo.
Kuna watu wengi wana matatizo ya Miguu,hii
ni kwasababu anaweza akawa ametembea katika eneo ambalo ardhi yake
inamatatizo,labda ni ardhi iliyobeba ushirikina au laana au magojwa,na kwa
sababu namna Mungu alivyoumba miguu yako ni kwaajili ya kumiliki,unajikuta kwa
kule kukanyaga katika ardhi ya namna hiyo unamiliki pamoja na magonjwa,laana na uchawi .hii ndio
sababu unahitaji kufanya maombi ya ukombozi mara kwa mara wa miguu yako.
Mungu alipoilaani ardhi katika mwanzo
3:17 maisha ya adamu yalikuwa ni
magumu,hii ni kwasababu miguu yake ilimiliki laana iliyokuwa katika ardhi.
habari njema ni kuwa Leo unakwenda
kufunguliwa katika jina la Yesu.
maelekezo
ya kinabii: chukua maji katika Beseni yaombee yawe Damu ya yesu, halafu nawa nyayo zako za miguu,Baada ya
maombi haya chini.
Maombi:
-
Baba kwa damu ya
thamani ya Yesu kristo,ninaomba utakaso wa Miguu yangu,nyayo zangu katika jina
la Yesu
-
Kila kitu
kilichopenyezwa Na Adui katika nyayo zangu kupitia ardhi kiharibiwe sasa katika
jina la Yesu
ukiwa unaomba ombi hili anza kuosha
miguu yako,au kama upo na familia kuhani wa familia afanye hiyo kazi na kisha
ajioshe mwenyewe.
-
ninatakasa kwa damu ya
Yesu lango langu la umiliki kwa miguu na kupitia Damu Yesu ,kila sumu iliyoko
katika miguu yangu iharibiwe kabisa katika Jina la Yesu.
2.Miguu
kama silaha
efeso
6:15
“na
kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
Luka
10:19
“Tazama,
nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala
hakuna kitu kitakachowadhuru.
Mungu anatuonesha jambo hapa ya kuwa
kupitia miguu unaweza kujipatia ushindi kamili katika maisha yako
Mamlaka ya kukanyaga sio kushika ni
kukanyaga kwa nyayo zako mamlaka za shetani,hii ni kukuonesha kuwa kupitia
miguu yako Mungu anaweza kuudhibiti utawala wa shetani katika maisha yako.
Mwanzo
3:15
“nami
nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake;
huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
ni
mpango wa Mungu kutumia miguu yako katika kuleta ushindi kwako na katika ufalme
wake,hii ndio sababu shetani nae hali akijua ya kuwa Mungu ameachilia uwezo wa
kivita katika miguu yako,haachi kuhakikisha anaharibu hiyo asili ya uwezo wako
watu
wengi katika ulimwengu wa roho miguu wanayotembelea sio ya kwao,wengine miguu
yao imebadilishwa na wamevikwa miguu ya aina nyingine,wengini miguu yao
imechukuliwa mateka ndio sababu hawawezi tena kuitumia miguu yao kwaajili ya
kumiliki ,
DALILI
ZA MIGUU ILIYOCHINI YA UVAMIZI
1. kukosa
nguvu
2. kuuma
mara kwa mara hasa katika nyayo
3. kuumwa
kichwa mara kwa mara
4. kuota
ndoto unakimbizwa na huwezi kukimbia
5. kuota
umekanyaga peku chooni au unakanyaga miiba
6. kuvimba
miguu
Maelekezo ya
kinabii: Chukua maji katika beseni changanya na
damu ya Yesu,kisha loweka miguu yako ndani na omba maombi haya kwa imani.
1. Baba
kwa damu yako ya thamani ninaomba rehema kwa kuruhusu adui kunyanganya mamlaka
iliyoko katika miguu yangu.
2. kwa
damu ya Thamani ninaikomboa miguu yangu
mahali popote ilipofungwa,kutekwa au kuibiwa katika Jina la Yesu
3. ninatuma
Moto na radi katika magereza yote ya kiroho mahali ambapo miguu yangu
imefungiwa
4. ninaharibu
kila mapepo yaliyoko katika miguu yangu kwa damu ya Yesu,kila pando
lililopandwa katika miguu yangu na nyayo zangu ambalo baba hajalipanda
ling’olewe sasa katika jina la Yesu.
5. ninatangaza
chini ya upako wa Roho mtakatifu ya kuwa niko huru kabisa.
UKOMBOZI KUTOKA KATIKA VIFUNGO VYA NAFSI
Nafsi
ni eneo ambalo lipo kati ya mwili wa Mtu na roho ya mtu,nafsi ninahusisha
maeneo matatu muhimu katika kumfanya mtu kuwa hai,ambayo ni akili,utashi na
Moyo
Akili: ndio mahali
yanapofanyika maamuzi na majadiliano kwaajili ya hatima ya maeneo mengine ya
Mtu, akili ya mtu inapokuwa ni njema na maisha yake huwa mazuri
utashi:,ni
mahali ambapo ndipo haiba ya mtu hupatikana ikiwamo tabia,na ule uwezo wa
kujitambua kuwa wewe ni nani na nini unahitaji kufanya,lakini pia hapa ndio
mahali mtu hutofautishwa na mnyama.
Moyo: ndipo mahali
vinapohivaziwa vitu vyote vinavyoingia kupitia milango ya fahamu,hii ndio
sababu maandiko yanasema linda sana moyo wako kuliko vyote uvilindavyo kwa kuwa
humo kunatoka chemichemi ya uzima
mathayo
15:19
Kwa maana moyoni
hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na
matukano;
sasa
nafsi ya mtu inaweza kufungwa,au kuibiwa au kuharibiwa kwa sababu shetani
anaamri juu ya mwili wako na nafsi yako lakini hana amri ya roho yako. Nafsi ya
mtu inaweza kushambuliwa na mapepo katika mazingira ya aina tatu
1. mapepo
yanaweza kumshambulia mtu yakiwa ndani yake
2. mapepo
yanaweza kumshambulia mtu yakiwa nje ya Mtu
3. mapepo
yanaweza kumshambulia mtu yakiwa yameambatanishwa au kushikishwa na nafsi ya
Mtu.
1.
MAPEPO
NDANI YA NAFSI YA MTU.
mapepo
yanapokuwa ndani ya nafsi ya mtu yanakuwa yanaendesha shughuli zote zinazohusu
nafsi,yaani akili yake inakuwa na mapepo na mtu huyu hataweza kabisa kufikiri
kwa kutumia akili yake aliyopewa na Mungu,hapa ndo unaona mtu alikuwa na akili
sana mara gafla akili yake imepotea dalasani, mtu huyu hata weza kuwa na utashi
ambao aliumbiwa,namna ya haiba yake huingiliwa na adui,ndio sababu utaona hata
jinsi anavyoonesha tabia yake ni ajabu ajabu,pia mtu ambaye ndani ya nafsi yake
kuna mapepo,utaona ya kuwa hata mawazo yaliyoko ndani ya moyo wake ni mabaya
tu,na kinachohifadhiwa ndani yake si
chema
unapokutana
na Mtu wa namna hii unajua tu ya kuwa ndani ya nafsi yake kumetawaliwa na
mapepo.
mfano:marko
5:1
Wakafika ng'ambo ya
bahari mpaka nchi ya Wagerase. 2Na
alipokwisha kushuka katika mashua, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka
makaburini, mwenye pepo mchafu; 3makao
yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu yeyote aliyeweza kumfunga tena,
hata kwa minyororo; 4kwa
sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile
minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za
kumshinda. 5Na
sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na
kujikatakata kwa mawe
2. MAPEPO
NDANI YANAYOSHAMBULIA KUTOKEA NJE YA NAFSI YA MTU
kuna
mtu mwingine ndani yake hakuna mapepo lakini napepo yanakua yanamshambulia kwa
nje ya nafsi yake,mtu huyu maisha yake huwa ni ya kubadilika badilika,kuna
wakati anakuwa na akili,kuna wakati hamna akili,kuna wakati anakuwa na haiba
nzuri,kuna wakati anakuwa kama mwehu,kuna wakati anakuwa na mawazo mazuri,kuna
wakati mawazo yake ni mabaya tu. mtu wa hivi hata maisha yake huwa ni ya
kuanguka na kusimama
1
samwel 16:23
Ikawa, ile roho mbaya
kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi alipokishika kinubi na kukipiga
kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
huu ni mfano wa Mtu
ambaye nafsi yake hushambuliwa na mapepo kutokea kwa nje,mara nyingi mtu huyu
anaweza akawa ameokoka na kwa sababu hiyo mapepo hayawezi kukaa ndani yake
hivyo roho chafu huja na kuondoka,mfano mtu anaweza akawa ni mgonjwa akiwa
nyumbani lakini akifika kanisani anakuwa mzima wa afya.
3.
MAPEPO
YALIYOSHIKISHWA NA NAFSI YA MTU.
kuna
watu wengine nafsi zao huwa zinakuwa zimeshikishwa na nafsi nyingine,utaona
mfano katika maandiko haya
1samweli
18:1
Ikawa Daudi
alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi,
Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. Sauli akamtwaa siku ile, wala
hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. 3Nao
Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. 4Ndipo
Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata
na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
Nafsi(roho)
ya yonathani iliambatana na ya daudi,maana yake ni kuwa nafsi ya daudi na ya
yonathani zilifungaanishwa ndani ya agano la upendo,hii ndio sababu unaona kuna
wakati yonathani alikuwa akimgeuka hata baba yake kwa kushirikisha taarifa za
siri kwa Daudi
kuna
mapepo ambayo yanaweza kufungwanisha na nafsi ya Mtu,mtu ambaye nafsi yake
imefunganishwa na mapepo,wakati mwingine hawezi kuwa na maamuzi ya kwake
mwenyewe,hawezi kujitawala,na siri zake za ndani hutambulikana na mapepo na
hivyo kujikuta njia zake za mafanikio zikijulika na kuzuiliwa.
wakati
mwingine unaweza ukawa umefungamanishwa kiagano na nafsi ya mtu ambaye
anamapepo,hivyo hata kama wewe huna mapepo unaweza ukajikuta unaambukizwa roho
za rafiki yako aliye na mapepo maandiko yanasema.
amosi
3:3
Je! Watu wawili
wanaweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
NJIA AMBAZO MAPEPO HUZITUMIA KUJIPENYEZA KATIKA
NAFSI YAKO.
1.
KUPITIA
URAFIKI
1samwel
18:1
Ikawa
Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya
Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.Sauli akamtwaa siku ile,
wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. Nao Yonathani na Daudi
wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. 4Ndipo
Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata
na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
mtu
anapofika katika eneo hili la urafiki,kuna mategemeo ya aina mbili,kwanba urafiki
huu unaweza kumpa faida au kuharibu kabisa maisha yake,kwa sababu nafsi
zinapoungana kupitia upendo zinafika katika kiwango cha kufanana,hii ni kwa
sababu kuna vitu ndani ya nafsi vinahama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwingine,hii ndio sababu maandiko yanasema.
2cor
6:14
Msifungiwe
nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki
gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena
pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?Beliari maana
yake ni, Ufisadi.
Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
Biblia
inasema msifungiwe nira na wasio amini,hii ni kwa sababu unapojenga urafiki wa
upendo pamoja na mtu asiyeamini,inapelekea kufungwa pamoja kinafsi na hivyo
kushirikiana viungo vya nafsi(tabia),unapokuwa na marafiki wengi wa kidunia si
ajabu maisha yako yakaanza kurudi nyuma kiroho kwa sababu ya impact ya nafsi
zao kwako.
2.
KUPITIA
TENDO LA NDOA
tendo
la ndoa huunganisha nafsi mbili kuwa moja maana yake ni kuwa kama mwanaumea
ndani yake kulikuwa na mapepo ya aina Fulani na mwanamke alikuwa na mapepo au
roho za aina Fulani wanapokutana kimwili huunganisha nafsi zao/mapepo yao na
kuyafanya kuwa na nguvu ya kutawala maisha yao, kama ni Baraka hivyo hivyo
huunganishwa
1cor
6:16
Au
hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale
wawili watakuwa mwili mmoja. 17Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
Unaona
yeye alalaye na kahaba ameunganishwa naye,unapolala na mwanamke au mwanaume
nafsi zenu zinaungana,na zinapoungana mtaanza kushare(kushirikishana) tabia
zenu,Baraka zenu,laana zenu n.k na huu ndio mlango mkuu wa mapepo hasa kwa
vijana. wengi hatima zao huharibiwa kwa namna hii,wanapolala na
wanawake/wanaume wenye mapepo.
Mithali
6:31
Mtu aziniye na mwanamke hana akili
kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza
nafsi yake.
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
Wala fedheha yake haitafutika.
unaona
hapo mwanzo nilisema mapepo yanapokaa ndani ya nafsi ya mtu huharibu akili
yake,na unaona maandiko yanasema alalaye na mwanamke(asiye wake) hana akili
kabisa,hii ni kwa sababu ukilala na mwanamke ambaye ni kahaba yale mapepo
huingia katika nafsi yako kupitia muunganiko wenu na kukukontrol kila kitu
ndani ya nafsi yako na kuharibu kabisa mfumo wako wa kufikiri.
3.
KUPITIA
VITU UNAVYOVIPENDA KUANGALIA AU KUSIKIA
Uaweza
ukawa unapenda aina Fulani ya vitu,labda miziki ya kidunia,au picha za ngono,au
filamu za aina mbalimbali,kumbuka hapo mwanzo nilikuambia ya Kuwa kazi ya moyo
ni kupokea na kuhifadhi kila kitu kinachopita katika milango yako ya fahamu na
kisha kukitoa nje,hii ndio sababu maandiko yanasema ndani ya moyo hutoka mawazo
mabaya.
sasa
kama unasikiliza nyimbo ambazo ndani yake zimefungamanishwa na mapepo,au
unaangalia filamu ambazo ndani yake zimefungamanishwa na mapepo,huingia ndani
ya moyo wako na kuharibu kabisa mfumo wa nafsi yako.
katika
kurasa za mwanzo niliandika ya kuwa wakati mwingine mapepo huingia ndani ya mtu
kupitia kuona hii ndio sababu ayubu aliweka agano na macho yake.
zaburi
119:37
Unigeuze macho yangu nisitazame
visivyofaa,
Unihuishe katika njia yako.
DALILI
ZA MTU AMBAYE ANAFSI YAKE IMEVAMIWA NA MAPEPO
1. kupoteza
kumbukumbu mara kwa mara
2. kukosa
uwezo mzuri wa kufikiri
3. kuwa
na mawazo mabaya mfano,mwawazo ya kiuasherati,kujiua,n.k
4. kuinuka
na kuanguka anguka katika wokovu na maisha
5. kuwa
na ndoto za kutisha mara kwa mara
6. ukichaaa,uwazimu
7. hasira
na uchungu uliopitiliza
8. hofu
na mashaka ya mara kwa mara
9. ulevi
wa vitu mbalimbali (addiction)
10. Tabia
mbaya(bad Character)
11. hali
ya kukata tama haraka
inawezekana
wewe ni muhanga wa hayo ambayo nimeyaonesha hapo juu,inawezekana upo katika
eneo moja wapo.habari njema ni kuwa Unaweza kufunguliwa kabisa katika hayo
maeneo tafadhali fuata Maelezo yaliyopo hapo chini.
maelekezo ya kinabii:
chukua mafuta ya ukombozi kisha paka katika kichwa chako pamoja na katika moyo
wake(eneo la nje kifuani) halafu anza kuomba maombi haya.
1. Baba
katika Jina la Yesu ninaomba Toba na msamaha juu ya kila jambo ambalo
nimelifanya kwa kujua au kutokujua ambalo limeruhusu mapepo kupata uhalali wa
kuishambulia au kukaa katika nafsi yangu.
2. katika
damu ya yesu ya thamani ninajifungua kutoka katika vifungo vyote vya nafsi
yangu nilivyojifunga mwenyewe au ninilvyofungiwa na mapepo kwa kujua au
kutokujua
3. Kwa
moto wa roho mtakatifu uteketeze kila mapepo yaliyokaa ndani ya moyo
wangu,ndani ya akili zangu na ndani ya utu wangu katika jina la Yesu
4. kila
aina za roho zilizofunganishwa na nafsi yangu kutoka kuzimu ziharibiwe sasa
kwamoto wa Roho mtakatifu katika jina la Yesu
5. kila
ndoto ambazo ni milango ya kipepo katika maisha yangu zihribiwe kabisa kwa jina
la Yesu
6. Ninarejesha
nafsi yangu na sehemu zake katika ukamilifu wake katika jina la Yesu
7. Damu
ya yesu inene mema katika nafsi yangu katika Jina la Yesu
8. ka
damu ya yesu najipatanisha nafsi yangu na nafsi ya Mungu leo katika jina la
Yesu.
Asante
Yesu niko huru.
NB:
Fika kanisani kwetu uonane na Nabii ili akupe maelekezo zaidi na kukuombea.
KUFUNGULIWA
KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA MADENI
2 falme
4:-5
Basi,
mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema,
Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa
mcha BWANA; na aliyemdai amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.
Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema,
Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta. Akasema, Nenda,
ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime
vichache. 4Kisha
uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile
vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.
Madeni
ni roho sio kitu cha kawaida cha kuzoeleka, Biblia inasema “ mdaiwa ni mtumwa wa anayedai”. Hii inamaana
mtu anayekudai anaweza kukutumikisha anavyotaka, atakuwekea masharti
anayoyataka yeye na utayafuta sababu uko chini ya deni. Anayekudai atakuwekea
hata kiwango cha ukomo cha amani yako, Hii ndiyo sababu unapokutana na mtu
anayekudai moyo wako unakosa amani.
Wapo
wengi wamehama makanisa Kwa sababu ya kudaiwa. unajisikiaje unapokaa ikaribu na
mtu anayekudai wakati wa kumwabudu Mungu kanisani?. Hii ndiyo sababu Mungu
anasema Kumb 28 “utakopesha wala hutakopa”.
Sio
watu wengi hutazama madeni kama roho, ndiyo sababu ni rahisi kunaswa katika
mkono wa madeni. Roho ya madeni
haichagui mtu wa kumvaa na kumwendesha, haijalishi ni mtu mkubwa au mdogo,
maskini au tajiri unapovamiwa na roho hii unakuwa mtumwa. Kuna watu ambao
hawawezi kuishi bila kudaiwa, hata kama hawapendi kwasababu hii ni roho,
itahakikisha baada ya kupata fedha unatumia haraka ili ukope tena, itahakikisha
ukishalipa deni unakuwa na kiu ya kukopa tena.
Sasa
maandiko hapo juu ya utaona kuna mtu aliitwa Elisha na alikutana na mmoja wa
wake za manabii ambaye mume wake alifariki. Mama huyu alikuwa anadaiwa katika
namna ambayo kama asingeweza kulipa watoto wake wangishia utumwani. Ndipo
alipokutana na Elisha nabii ambaye aliachilia Neema ya utele iliyoshinda roho
ya madeni. Hii inatudhihirishia ya kuwa mtu anaweza kutoka katika roho ya
madeni kwa Neema ya Mungu inayoleta utele. Habari njema ni kuwa leo roho ya
madeni itakomeshwa kabisa kwenye maisha yako katika jina la Yesu Kristo.
maelekezo
ya kinabii ya I
Chukua Mafuta ya Upako (
Anointing Oil) kisha jipake kichwani kwako huku ukiomba maombi haya;(isaya 10:27)
1.
Baba
katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba kwa damu yako kufutika kwa kila deni
katika maisha yangu.
2.
kila
nira na mzigo wa Madeni katika maisha yangu uharibiwe katika Jina la Yesu.
3.
Ninakemea
na kuharibu kila roho ya madeni katika maisha yangu na watoto wangu, ninaiamuru
iniachie kwa Jina la Yesu Kristo. (sema niachie kwa Jina la Yesu kwa sauti mara
7).
Maelekezo ya kinabii II
Chukua
kitu chochote kinachowakilisha chanzo chako cha kipato kisha anza kuomba maombi
haya
1.
Kwa
Jina la Yesu Kristo, Imeandikwa nimewekewa mlango wazi mbele yangu wala hakuna
awezaye kuufunga. Hivyo kila mlango wa kipato uliofungwa au kuminywa naamuru
ufunguke katika Jina la Yesu Kristo.
2.
Ninaamuru
Baraka ya Utele kuja juu yangu na familia yangu kwa Jina la Yesu Kristo.
3.
Ninakataa
kukopa, bali nitakopesha katika Jina la Yesu Kristo.
N.B
Baada ya maombi haya Mungu amefungua milango yako, Hivyo hakikisha unafanya
yafuatayo
·
Fedha
inayokuja mkononi mwako tumia kulipa madeni.
·
Hakikisha
kama unafanya kazi/ biashara unatoa fungu la kumi na dhabihu kwa BWANA ili
apate kukuzidisha. kumb 8:18, malaki 3:10
------------ASANTE YESU MKO
HURU----------
hakikisha
unaendelea kufanya maombi ya ukombozi mara kwa mara,na kuanzia katika kurasa
zinazofuata nimekuwekea maombi mengine ya ukombozi ili yakusaidie unapoendelea
kuomba kwajili ya maisha yako.
MAOMBI
YA UKOMBOZI.
1.
Ninarudisha mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/mababa, katika Jina la
Yesu.
2.
Nina zilaani roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano katika maisha
yangu na naziamuru kuniachia kwa Jina la Yesu[ Sema mara 3 na anza kusema
hivi,”niachie kwa jina la Yesu
3.
Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo,
ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu
4.
Kila aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa,
katika jina la Yesu, nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5.
Ee Bwana Yesu,shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu,iliyoandaliwa kwa
ajili yangu, katika jina la Yesu
6.
Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho, katika jina la
Yesu
7.
Upanga wa moto, na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi, katika jina
la Yesu
8.
Ee Bwana, nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu
au anataka kufunga na nafsi yangu, katika jina la Yesu.
9.
Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu, nina
kungo’a katika jina la Yesu.
10.
Baba nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu
yangu lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.
11.
Agano lolote la siri ambalo ni la uovu, ninakuvunja katika jina la Yesu
12.
Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote
13.
[Imba wimbo huu kama unaweza, kama huwezi usilazimshe: Kuna nguvu ya ajabu,
damuni mwa Yesu ]
14.
Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu
15.
Ee Bwana, badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka
16.
Kila nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu, ninakuamuru kurudi moja kwa moja, kwa
mtumaji katika jina la Yesu.
17.
Ee Bwana Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika
maisha yangu, kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.
18.
Nina jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na
adui,katika jina la Yesu.
19.
Nina jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina
la Yesu.
20.
Ee Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na
uharibu/ulikate kila pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.
21.
Nina ipitisha Damu ya Yesu, katika mifumo yote ya mwili wangu [mfumo wa damu,
wa fahamu, wa chakula, wa upumuaji, wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote
ya urithi wa vitu viovu katika jina la Yesu.
22.
Damu ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu
[Figo, moyo, mapafu, macho, masikio, n.k] katika jina la Yesu
23.
Nina vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina
la Yesu.
24.
Nina jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika jina la
Yesu
25.
Nina tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha yangu, katika
jina la Yesu
26.
Mapepo, majini, mizimu na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na
mpararaizi[mpooze] sasa katika jina la Yesu.
27.
Shambulio lolote lilopangwa juu ya familia yangu, ninalibatilisha kwa ajili
yangu katika jina la Yesu
28.
Nina vunja matoke mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu, lilipachikwa kwenye
nafsi yangu katika jina la Yesu
29.
Nina batilisha laana zote, mikosi, majanga, ajali, maradhi yote yaliyoelekezwa
kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
30.
Muombe Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya
kutotii neon lake[kumb 28:]
31.
Pepo lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi, toka, katika
jina la Yesu
32.
Laana zote katika maisha yangu, badilika na kuwa Baraka, katika jina la Yesu
33.
Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa hapo chini, sema kwa kumaanisha
“vunjika, vunjika, vunjika” katika jina la Yesu. Nina jitenganisha na nyinyi
katika jina la Yesu.
•
Laana zote za udhaifu wa kiakili na kimwili
•
Laana zote za kushidwa katika kila ninalofanya
•
Laana zote za umaskini
•
Laana zote za kuvunjika kwa familia
•
Laana zote za kuonewa na kudharauliwa
•
Laana zote za Uharibifu wa mtu binafsi,kama vile kujinyonga n.k
•
Laana zote za magonjwa sugu
•
Laana zote za kishirikina
•
Laana zote za kuharibikiwa mambo ya uzazi na viungo vya uzazi
•
Laana zote za kufanya kazi kwa bidii pasipo kuiona faida
•
Laana zote za kulowea mambo ya uovu kama vile zinaa, pombe, sigara n.k
34.
Jitamkie maneno ya Baraka wewe mwenyewe, kwa mfano kwa kusema “hakutakuwa na
umaskini tena, magonjwa tena n.k katika maisha yangu katika jina la Yesu.
35.
Nina jifungua na kujitenganisha na vifungo vya madhabahu zote za giza katika
jina la Yesu.Sema mara kadhaa ukifuatiwa na maneno yafuatayo “nina
jitenganisha” katika jina la Yesu.Tumia muda kidogo kwenye hilo.
36.
Nina tapika sumu zote za mashetani nilizozimeza katika jina la Yesu.
37.[Weka
mikono yako juu ya kichwa chako] Nina vunja kila mamlaka za giza katika maisha
yangu, katika jina la Yesu.Rudia “nina vunja katika jina la Yesu.
38.
Taja mambo yafuatayo kwa mamlaka na sema “vunjika kwa jina la Yesu.
•
Mamlaka zote za mizimu na miungu ya familia, ukoo, na kabila
•
Mamlaka zote za roho za kichawi zilzopo ndani ya familia, ukoo, kabila
•
Mamalaka zote zilizoshika rimoti za kudhibiti familia, ukoo, kabila
•
Mamlaka zote ovu ndani ya Familia, ukoo, kabila nk
39.
Kila mmiliki wa mzigo niliobebeshwa beba mzigo wako katika jina la Yesu[Mzigo
unaweza kuwa ugonjwa,mikosi wabebeshe wamilki]
40.
Nina zipoodhesha/nina zipararaizi madhabahu zote za giza katika jina la Yesu
41.
Nina zilaani madhabahu zote za uovu zilizoelekezwa zidi yangu katika jina la
Yesu
42.
Nina agiza nyundo ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi,iponde kila madhabahu ya
giza zilizoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
43.
Ee Bwana tuma moto wako na uteketeze madhabahu zote za giza zinazoinuka dhidi
ya maisha yangu,
44.
Makuhani wote wa madhabahu zote za giza wanaocheza na maisha yangu,wakutane na
upanga wa roho mtakatifu. Katika jina la Yesu.
45.
Mkono wowote unaotaka kunikamata na kuniteka kwa ajili ya Maombi haya
ninayoomba kauka katika jina la Yesu.
46.
Nina waamuru makuhani wa madhabahu za giza kunyweni damu wenyewe katika jina la
Yesu
47.
Nina rudisha urithi wangu ulioibiwa na madhabahu za giza katika jina la Yesu.
48.
Ninafuta/ninaliondoa jina langu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
49.
[Weka mkono wako mmoja kifuani] Ninaziondoa Baraka zangu kwenye madhabahu za
giza katika jina la Yesu
50.
[Weka mkono mmoja kifuani na mwingine kichwani] Ninaondoa kitu chochote kile
kinachoniwakilisha mimi [kama vile nguo] kwenye madhabahu za giza katika jina
la Yesu.
51.
[Taja kiungo chochote katika mwili wako ambacho akifanyi kazi ipasavyo au kama
ni mwili wote taja mwili] na useme maneno yafuatayo “nina kuondoa kwenye
madhabahu za giza” katika jina la Yesu. Tamka hivyo mara saba.
52.
Nina jitenganisha kutoka kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza katika
jina la Yesu
53.
Damu ya Yesu na unene kwa ajili yangu dhidi ya maagano yote na nguvu za giza
54.
Nina tamka Uharibifu dhidi ya roho chafu zote katika maisha yangu.Katika Jina
la Yesu.
55.
Nina jitenganisha na laana zote za maagano katika jina la Yesu
56.
Nina jitenganisha mimi na familia yangu kutoka katika kila agano la damu katika
jina la Yesu.
57.
Ninajitenganisha na kila agano la damu la kurithi katika jina la Yesu.
58.
Nina iondoa damu yangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
59.
Nina iondoa damu yangu kutoka kwenye benki za damu kwenye ulimwengu wa giza
katika jina la Yesu
60.
Nina vunja kila agano la damu la kutokukusudia kwa jina la Yesu
61.Ee
bwana, damu ya mnyama yeyote iliyomwagika kwa niaba yangu, Naipoteze nguvu ya
agano sasa, kwa jina la Yesu
62.
Kila tone la damu linalotamka mabaya dhidi yangu, na ikae kimya sasa, kwa damu
ya Yesu
63.
Ninajifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila agano la damu la kifamila, kiukoo,
kabila katika jina la Yesu.
64.
Nina jitenganisha na kila agano la damu nililoingia kwa kujua au kutojua kwa
jina la Yesu
65.
Ee Bwana kila agano la damuna nguvu za giza lipoteze nguvu na uhalali wake juu
yangu katika jina la Yesu.
66.
Damu ya agano jipya la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo, naiikemee damu ya
agano na nguvu za giza ilijipanga kinyume name. Kwa jina la Yesu
67.
Nimepewa mamlaka ya kubatilisha haki zote zilizopo kwenye maagano yote ya damu
na nguvu za giza .kwa jina la Yesu.
68.Agano
lolote la damu na nguvu za giza lililofungwa kwenye kiungo chochote kwenye
mwili wangu, nalivunjike sasa.Kwa jina la Yesu
69.
Ninapokea vitu vyote vilivyoibiwa au kuchukuliwa na adui kupitia maagano na
nguvu za giza. Kwa jina la Yesu.
70.
Nina vunja agano lolote la damu na nguvu za giza kwenye damu yangu . Kwa jina
la Yesu
No comments:
Post a Comment