KUBOMOA MADHABAHU ZA SHETANI(Samson Mollel


KUBOMOA MADHABAHU ZA SHETANI(Samson Mollel – Uzima wa Milele International Ministries) (Somo limefundishwa na Bishop J. Gwajima – Kitabu cha Maombi ya Kubomoa Madhabahu)
Madhabahu ni nini?
Ni daraja la kuunganisha katika ya ulimwengu wa roho wa Mungu au shetani.
Kuna aina 2 za madhabahu, Madhabahu ya MUNGU (Nuru)na madhabahu ya shetani (giza)

***MADHABAHU YA MUNGU
Watu/watumishi wa Mungu katika Biblia walianza kwa kujenga madhabahu kabla ya kufanya chochote

NUHU – Mwanzo 8:20“Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.”

MUSA – Kutoka 17:15“Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;”

YOSHUA – Yoshua 8:30“Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali.”

GIDEONI – Waamuzi 6:24“Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”

SAMWELI – 1 Samweli 7:17“Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhabahu.”

***MADHABAHU YA SHETANI
shetani na watumishi wake wana madhabahu ambayo hutumia kupitisha mambo mabaya/maovu kutoka katika ulimwengu wa roho (giza) kuingia katika ulimwengu wa mwili.
Kutoka 34:11-13 “11 Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 12 Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. 13 Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao.”
Mungu anawaagiza wana wa Israeli wasifanye maagano na wenyeji bali wabomea madhabahu zao kwani matatizo ili yakupate lazima yatokee katika madhabahu ya shetani.
Kumb 12:2-3 “2 Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; 3 nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.”

MAMBO MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU
1.      Mungu wa madhabahu
2.      Kuhani wa madhabahu
3.      Washirika wa madhabahu
4.      Kafara ya madhabahu
5.      Nguvu ya madhabahu

1.     MUNGU WA MADHABAHU
Neno “mungu” ni nafasi au cheo kama ilivyo kwa Rais. Kwa maana hiyo unapotaja jina la mungu inakubidi uainishe ni mungu yupi unayemtaja.
Kutoka 6:1-3“1 Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake. 2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.”

**MUNGU WA MADHABAHU ZA KISHETANI
shetani ndiye mungu wa madhabahu za wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota na mawakala wote wa mauti.
2Kor 4:4“ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
1Wafalme 16:32“31 Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia. 32 Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria.”

*****FANYA MAOMBI YA KUWAANGAMIZA MIUNGU WA MADHABAHU ZA KISHETANI*****

2.     KUHANI WA MADHABAHU
Kuhani wa madhabahu ni mtu mwenye uwezo wa kuleta mambo kutoka ulimwengu wa roho kuingiza katika ulimwengu wa mwili.
Mwanzo 14:18 “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.”

**KUHANI WA MADHABAHU ZA KISHETANI
1 Samweli 5:5 “Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.”
1Wafalme 18:25-26 “25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. 26 Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.”

**** FANYA MAOMBI YA KUWAANGAMIZA MAKUHANI WA MADHABAHU ZA KISHETANI

3.     KAFARA YA MADHABAHU
Madhabahu haiwezi kukamilika kama hakuna kafara kwasababu kila mungu wa madhabahu huhitaji kafara.

Walawi 2:2“kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana;”

Zaburi 40:6“6 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.”

Zaburi 50:8“Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima.”

**KAFARA KWENYE MADHABAHU YA KISHETANI

Zaburi 106:36-38“36 Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao. 37 Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani. 38 Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani; Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.”

Yeremia 32:35“Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.”

****MAOMBI YA KUANGAMIZA KAFARA ZA MADHABAHU ZA KISHETANI

4.     WASHIRIKA WA MADHABAHU
Washirika wa madhabahu ni watu muhimu sana kwenye madhabahu. Kama vile wewe ulivyo ni mshirika wa kanisa Fulani vivyo hivyo kila madhabahu ya kishetani inayo washirika wake.
Eliya alifahamu umuhimu wa kuwa na washirika. 1Wafalme 19:9-10“9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? 10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.”

Mungu anamtoa Eliya hofu 1Wafalme 19:18“Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.”

**WASHIRIKA WA MADHABAHU ZA KISHETANI
Hawa ni watu hatari sana, kwakuwa matatizo yote huanzia kwenye madhabahu za kishetani, wanao peleka jina lako/kazi yako/ndoa yako/elimu yako…… ni washirika wa madhabahu ili lijadiliwe kwa lengo la kuharibu maisha yako.

Washirika wa madhabahu ya kishetani mara zote ni watu wako wa karibu
Waamuzi 16:5 “Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.”

Mathayo 10:36“na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.” Na Mika 7:5-6“5 Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari. 6 Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na mavyaaye; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.”

****MAOMBI YA KUWAANGAMIZA WASHIRIKA WA MADHABAHU ZA KISHETANI

5.     NGUVU YA MADHABAHU
Nguvu ya madhabahu inategemea mambo yote yanayounda  madhabahu yaani Mungu wa madhabahu, kuhani wa madhabahu, kafara ya madhabahu na washirika wa madhabahu.
Mashetani walio katika madhabahu wanao mfumo wa uongozi wa kifalme. Imeandikwa Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

****FANYA MAOMBI YA KUHARIBU NGUVU YA MADHABAHU ZA KISHETANI

Isaya 47:9-12 “9 lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno. 10 Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi. 11 Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua. 12 Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.”


Ezekiel 13:17-22“17 Na wewe, mwanadamu, kaza uso wako juu ya binti za watu wako, watabirio kwa akili zao wenyewe; ukatabiri juu yao, 18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? 19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege. 21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 22 Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia yake mbaya, na kuhifadhika; 23 basi, kwa sababu hiyo ninyi hamtaona tena ubatili, wala kutabiri mambo; nami nitawaokoa watu wangu katika mikono yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”

No comments:

Post a Comment