MALAIKA BY PROPHET KELVIN RAPHASON


ANGELS
MALAIKA


Ezekiel 1
Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo. 5Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu. 6Na kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. 7Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana. 8Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi; 9mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele. 10Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng’ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia. 11Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili yalifunika miili yao.Nao walikwenda kuelekea mbele, kila mmoja wao; roho ilikotaka kwenda ndiko walikokwenda; hawakugeuka walipokwenda. 13Kwa habari za kuonekana kwao vile viumbe hai; kuonekana kwao kulikuwa kama makaa ya moto yawakayo, kama kuonekana kwa vinga vya moto; moto ule ulikuwa ukienda juu na kushuka chini, katikati ya vile viumbe hai; na ule moto ulikuwa na mwangaza mwingi, na katika ule moto ulitoka umeme. Na vile viumbe hai walipiga mbio, kwenda na kurudi, kama kuonekana kwa kumulika kwa umeme. 15Basi, nilipokuwa nikivitazama vile viumbe hai, tazama, gurudumu moja juu ya nchi, karibu na kila kimoja cha vile viumbe hai, pande zake zote nne. 16Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine. 17Yalipokwenda yalikwenda pande zote nne; hayakugeuka yalipokwenda. 18Katika habari za vivimbe vyake; vilikuwa virefu, vya kutisha; nayo yote manne, vivimbe vyake vimejaa macho pande zote. 19Na viumbe hao walipokwenda, magurudumu yalikwenda kandokando yao, na viumbe hao walipoinuliwa, magurudumu nayo yaliinuliwa. 20Kila mahali ambako roho hiyo ilitaka kwenda, walikwenda; walikuwa na roho ya kwenda huko; nayo magurudumu yaliinuliwa karibu nao; kwa maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu.21Walipokwenda hao, yalikwenda hayo nayo; na waliposimama hao, yalisimama hayo nayo; na walipoinuliwa hao juu ya nchi, magurudumu yaliinuliwa karibu nao; maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu. 22Tena juu ya vichwa vya viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa anga, kama rangi ya bilauri, lenye kutisha, limetandwa juu ya vichwa vyao. 23Na chini ya anga mabawa yao yamenyoshwa, moja kulielekea la pili; kila mmoja alikuwa na mawili yaliyowafunika miili yao upande mmoja, na kila mmoja alikuwa na mawili yaliyowafunika miili yao upande wa pili. 24Nao walipokwenda nalisikia mshindo wa mabawa yao, kama mshindo wa maji makuu, kama sauti yake Mwenyezi, mshindo wa mvumo, kama mshindo wa jeshi; hapo waliposimama walishusha mabawa yao.25Tena palikuwa na sauti juu ya anga lile, lililokuwa juu ya vichwa vyao; hapo waliposimama walishusha mabawa yao. 26Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake. 27Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote. 28Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nalianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.








ASILI YA MALAIKA
MALAIKA NI ROHO
Hebrew 1:14
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Asili ya malaika ni asili ya kiroho,hii inamaana ya kuwa malaika hawana mwili kama sisi,tofauti yetu na malaika katika uasili ni kuwa malaika wao ni roho wakati sisi ni roho ndani ya mwili,wakati wao waliumbwa na hawawezi kuzaliana kulingana na eneo la utumishi wao,sisi tumeumwa na kukusudiwa kuzaliana kulingana na eneo letu la kusudi.
Kimsingi ni kuwa kila roho inauwezo wa kujizidisha kwa namna ya kuzaliana,hata malaika ambao ni roho kamili wana uwezo wa kuza kama vile  na roho ya mwanadamu ilivyo na uwezo wa wa kuzaa.tofauti kubwa huwa katika eneo/mahali roho hiyo ipo.najua wengine mnaweza jiuliza mbona kuna wakatifulani BWANA yesu aliwahi kuulizwa swali juu ya kuoa na kuolewa na jibu lake likawa mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa bali wote huwa kama malaika,sasa inawezekanaje malaika kama roho kuweza kuzaa?
Sasa kulijibu swali hili ni muhimu tukaangalia mstari wenyewe
Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu? Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.
Marko 12:25

Angalia maandiko yanasema mbinguni wote huwa kama malaika hajasema duniani, malaika wanapokuwa katika eneo la Mbinguni hawawezi kuzaa, kuoa ama kuolewa,hii haina maana hawawezi kuoa au kuolewa na pia haina maana hawawezi kuzaa,ni mazingira ya kieneo ndiyo huwafanya wasioe wala kuolewa.
Katika falme nyingi Duniani wahudumu wa mfalme wanaokaa katika ikulu ya mfalme au nyumba zilizopo ndani ya ikulu huwa hawaruhusiwi kuoa au kuolewa na huitwa matowashi,japokuwa hii haimaanishi kuwa hawana uwezo wa kuoa au kuolewa na kuzaa.hebu tuangalie mfano.
Mwanzo 6:
Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.

Mistari hii inazungumza juu ya wana wa Mungu wa kimalaika (angels) ambao walikuwa katika dalaja la kwanza la mbingu (maana kuna mbingu tatu 2 korth 12)
Aina hii ya malaika wanaitwa malaika waangalizi (guardian Angels), walipokuwa wakitazama Dunia kwa wakati huo wakawaona binti za wanadamu, wakatamani kuishi katikati ya wanadamu ili waoe na kuwa na watoto. Na hii ndio sababu kuna uzao mwingine usio wa kibinadamu ukatokea Duniani ambao ni uzao wa kinefili.

Jambo hili halikutokea mbinguni,lilitokea duniani,Duniani ndio  mahali pekee ambapo viumbe vinauwezo wa kuzaa na kuzaliana,ni eneo ambalo hata katika kuumbwa kwake liliumbwa kama sehemu ya kuzalishia wana wa Mungu.
Lengo la kukuleta mpaka huku ni ili kukuonesha ya kwamba malaika kama roho wanauwezo wa kuzaa lakini ni pale tu wanapokuwa duniani na si wanapokuwa mbinguni.
Namna walivyoumbwa
Biblia haisemi chochote juu ya namna malaika walivyoumbwa na hakuna record yoyote inayoelezea jinsi walivyoumbwa isipokuwa Biblia inasema waliumbwa kabla ya Dunia kuumbwa na ya kuwa malaika waliumbwa kama roho za utumishi (serving spirit) sio kama wana.
Ayubu 38:4
Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?
Haya! Sema, Kama ukiwa na ufahamu.
Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?
Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?
Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,
Na wana wote waMUNGU walipopiga kelele kwa furaha?

Ukiangalia mistari hiyo hapo juu utagundua ya kuwa MUNGU alipokuwa akiweka misingi ya dunia, malaika (wana wa MUNGU) walikuwepo wakishangilia kwa furaha kuu.
Lakini pia tunapoangalia ya kuwa katika bustani ya edeni maandiko yanasema shetani alikuwepo tayari katika sura ya nyoka (maana yake tayar aliuwa ameshaumbwa na ameishi katika umalaika kwa kipindi na kisha akaanguka na kutupwa duniani)
Mwanzo 3:1-3
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa

Ezekiel 28
Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.


Hebrew 1:14
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Kusudi lao la kuumbwa ni kutumika mbele za Mungu na kuwahudumia wana wa Mungu,hii inamaana ya kuwa katika daraja la utumishi mbele za Mungu Mwanadamu ametukuzwa zaidi ya malaika
Waebrania 1:1-14
Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote,
Ndiwe mwanangu,
Mimi leo nimekuzaa?
Na tena
Mimi nitakuwa kwake baba,
Na yeye atakuwa kwangu mwana?
Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,
Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.
 Na kwa habari za malaika asema,
Afanyaye malaika wake kuwa pepo,
Na watumishi wake kuwa miali ya moto.
Lakini kwa habari za Mwana asema,
Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele;
Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Umependa haki, umechukia maasi;
Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,
Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
Na tena,
Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,
Na mbingu ni kazi za mikono yako;
Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;
Nazo zote zitachakaa kama nguo,
Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;
Lakini wewe u yeye yule,
Na miaka yako haitakoma.
 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,
Uketi mkono wangu wa kuume
Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Lakini heshima hii ipo kwa wana wa mungu na si kwa wanadamu wote.
Yohana 1:12
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Ili uhudumiwe na malaika ni lazima uwe mtoto wa Mungu,na kuwa mtoto wa Mungu ni lazima uzaliwe mara ya pili kwa maji na kwa roho,hii ndio sifa ya kwanza ya kutumikiwa kama mfalme na mwana wa Mungu.
Mwanzo 24:7
BWANA, MUNGU wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke tokea huko

Katika biblia unaweza ukaona kila mahali ambapo palikuwa na watu wa MUNGU au pana kusudi la MUNGU ni lazima palikuwa na udhihirisho wa kimalaika
Kuanzia kitabu cha mwanzo mpaka ufunuo kila mahali utaona malaika wakihusishwa, na kila mahali amabapo malaika walihusishwa kuna mambo makubwa ambayo yalitokea.
Hii ndio sababu ibrahimu alipomtuma mtumishi wake kwenda kumtafutia mke Isaka alimuunganisha na malaika,hii ni kwa sababu swala kama hili haliitaji tu uchaguzi wa kimwili bali linahusisha pia uchaguzi wa kiroho,unaporuhusu usaidizi wa malaika katika kazi zako,huduma yako,au chochote unachofanya kuwa na uhakika kuwa kila kitu kitakwenda sawa.
Huduma ya Yesu ilikuwa na mafanikio si tu alikuwa mwana wa Mungu lakini pia ni kwa sababu katika kila hatua ya muhimu malaika kama wasaidizi walihusishwa, kuanzia kutangazwa kuzaliwa kwake mpaka katika kufufuka kwake.tunasoma.
Luka 1
Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Malko 1:13,
Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia.
luke 22:43
Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Hakuna namna unaweza ukafanikiwa katika maisha kama mtoto wa Mungu bila kuwahusisha viumbe hawa, ikiwa katika biashara au katika huduma malaika hufanya kazi kubwa katika kukuletea matunda
Ninakumbuka katikati ya mwaka 2007 nikiwa ninavuka barabara kuelekea shuleni wakati huo nikiwa kidato cha nne shule ya Airwing secondary, sikuwa nimeangalia vizuri barabalani na gafla wakati ninavuka kumbe gari ilikuwa tayari Miguuni Pangu, namshukuru MUNGU kwakuwa kabla gari kabla haijagonga miguu yangu nilirushwa kwa namna ya ajabu sana pembeni mwa barabara na kujikuta nikianza kuvuka tena. Halikuwa ni Jambo rahisi sana kwa akili ya kibinadamu,hii ilikuwa ni moja kati ya kazi za malaika katika maisha yangu.
Wakati mwingine nikiwa chuoni mimi na rafiki yangu Frank shayo tulikuwa tunaishi katika chumba tulichokuwa tumepanga maeneo ya uwanja wa ndege Dodoma,kuna wakati tungeweza kulala bila kufunga mlango wala kuchomeka chandarua,lakini ajabu tungeweza kuamka asubuhi na kuona mlango ukiwa umefungwa na tumechomekewa chandarua,ilikuwa ni ajabu sana,malaika wanaweza kufanya hata vitu vidogo vidogo ambavyo unadhani hawawezi kufanya .
1falme 19:5
Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. Malaika wa BWANA akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Wao ni roho wa utumishi haijalishi ni jambo gani ni kubwa kiasi gani au ni dogo kiasi gani, unaporuhusu wakusaidie utaona wakifanya kwa uaminifu kabisa.
Ni mara nyingi sana nimekuwa nikiona MUNGU akituma malaika kwaajili yangu na ninakutia moyo kuwa usione uko peke yako, hebu mwambie Baba atume malaika kwaajili yako.MUNGU BABA amewaweka kwa kusudi maalumu kwaajili yako.

UUMBWAJI WA MALAIKA NA MAUMBO YAO
Tumeshaona katika kurasa zilizopita ya kuwa malaika waliumbwa na ya kuwa wao hawazaliwi kama sisi kulingana na eneo lao la utumishi lakini pia kulingana na kusudi lao,lakini kama viumbe wengine wakiroho wanatabia na sifa zinazofanana kama zifuatazo.
1.      Malaika wana hisia.
Kama viumbe wengine walio umbwa na MUNGU, malaika pia wanahisia, maana yake wanajisikia vibaya lakini pia wanajisikia vizuri,wanaweza wakaumia na pia wanauelewa juu ya mambo mengi hata kuzidi mwanadamu wa kawaida,akili zao ziko juu pengine kuliko wanadamu wa kawaida,tunasoma
Kutoka 23:20
Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. 21Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake
Utaona malaika wana uwezo wa kukasirika, maana yake ndani yao wanazo hisia, malaika hukasirika pale ambapo wanamuhudumia mtu ambaye hufanya kinyume na mapenzi ya Mungu kwa makusudi,au mtu asiyesikia kile Mungu anasema.
Ndani ya malaika kuna sheria ya BWANA au JINA la BWANA, hii ina maana ya kuwa wao huongozwa na Neno au sheria ya Bwana,na MUNGU anapotuma malaika mbele kwaajili yako,ndani yao MUNGU anakuwa ameweka maagizo ya kukufikisha mahali ambapo unapotaka kufika,inapotokea ukawa ni mtu mwenye moyo mgumu au mwepesi wa kukata tama hata katika mambo madogo,kutokuwa msikivu,kutokutumia ufahamu wako ipasavyo,kutokuwa na imani,kutokuheshimu mwili wako n.k si tu kwamba unamkasilisha MUNGU bali unamkasirisha pia malaika anayefuatana na wewe.
Lakini pia utaona mahali pengine biblia inasema malaika mbinguni hufurahi pale mwenye dhambi mmoja anapotubu na kumgeukia Mungu.
Mathayo 15;7
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa Na furaha mbinguni Kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.


2.      Malaika wana milango ya fahamu.
Kama wanadamu vile vile malaika wana milango ya fahamu na pengine ni zaidi ya milango ya fahamau ya mwanadamu wa kawaida
Mwanzo 16:7
Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.
Pamoja na kwamba wakati mwingine unaweza ukahisi hakuna anayekuona ukiwa unafanya jambo, fahamu ya kuwa viumbe hawa malaika wanakuona na pia wanakusikia kila ambacho unakisema,hii ndio sababu biblia inasema huwezi kujificha mbele za Bwana
Zaburi 139:7
Niende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
Ningezitwaa mbawa za asubuhi,
Na kukaa pande za mwisho za bahari;

3.      Malaika wana viungo
Malaika wanaviungo japokuwa aina za viungo vyao vinaweza vikatofautiana na sisi pia katika ukubwa na utendaji kazi wake,


MAUMBILE YAO
Malaika wana maumbo mbalimbali ambayo yanategemeana na makusudi ya uumbwaji wao, kuna malaika ambao wanafanana na magurudumu ya magari(ofanim) wengini wana sura ya wanadamu,kuna wenye mabawa na wasio na mabawa ,tutaangalia zaidi tutakapofika katika kipengele cha aina za malaika
Lakini pia wakati mwingine maumbo yao hutegemeana na mazingira na kusudi la kazi wanazofanya.kwa lugha nyepesi ni kuwa malaika wanaweza kuvaa aina Fulani ya maumbo na wakaishi katika aina hiyo ya maumbo mpaka wakati wao wa kumaliza kusudi lao.

Mwanzo 6:1
Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

Utaona hawa malaika ambao hapo kwanza tuliwaangalia wenye majina ya waangalizi wa ulimwengu(guardians angels/the watchers) walipoazimia kufanya uovu kati ya wanadamu walivaa maumbo ya kawaida ya kibinadamu
Lakkini pia tunasoma juu ya malaika Gabliel alipokwenda kumtembelea mariamu ambaye baadaye alikuwa mama yake Yesu katika mwili alikuwa katika umbo la kibinadamu.

Luka 1:26
Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?

Ni kawaida ya mwanadamu kushangaa pale anapokutana na malaika wakiwa katika maumbo ya kiroho na wengine huzimia kabisa na kuwa kama wafu lakini hii haikuwa kwa mariam,isipokuwa tunaona mariam akishangaa salamu inayotoka kwa huyu malaika kwa sababu ni salamu ya kimalaika iliyotoka kwa mtu wa kawaida.
 Lengo langu hapa ni kuwa unahitaji kuwa na wigo mpana wa kimawazo juu ya maumbile yao kwa sababu unaweza ukawa umewaona na usitambue ya kuwa hawa ni malaika,hii ndio sababu Nabii na Mtume Paulo anasema
Waebrania 13:2
Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.






AINA NA KAZI ZA MALAIKA
KAZI ZA MALAIKA.
1.      Malaika huudumu katika Maombi kupeleka Maombi na kuleta majibu ya maombi.
Ufunuo 8:4
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, Ili autie pamoja Na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. 4Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. 5Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.
Wakati Mtu anapoomba Mungu hutuma malaika ili kukusanya maneno yake na kuyachanganya ndani ya chetezo kisha wakisha kamilisha utaratibu wote huyapeleka mbale za Mungu kama harufu ya manukato.
Hii ina maana ya kuwa maombi unayoyaomba mbele za Mungu huwa ni manukato na si maneno ambayo umeyasema,hii ni kwa sababu MUNGU haihitaji maeno yako ili kuruhusu jibu lako kwa sababu Mungu husikiliza moyo wako.
Isaya 65:24
Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
Labda nijaribu kuelezea namna hii ili tupate ufahamu kidogo juu ya namna maombi yanavyofanya kazi.
Kimsingi kile unachoomba leo sio ambacho Mungu anakwenda kukifanya kwa wakati huo,amaombi ni kama maono,kile unachoona leo si kama ndio kimetokea wakati huo,isipokuwa ni wewe ndio umepata afasi ya kuona hicho kitu katika ulimwengu wa roho,maana yake hicho kitu kilikuwepo tayari.
Sasa maombi majibu yake tayari yalishajibiwa kwa sababu kabla hujaomba Mungu anakuwa amesha jibu na ukiwa katika kunena ameshasikia,angalia  hili,wakati ulipokuwa unaumbwa katika Tumbo la mama yako Mungu alishafahamu tayari kuwa utazaliwa na ya kuwa utahitaji hayo unayoyaomba na kwa sababu hiyo kwa neno wake akaumba kila kitu na kukiweka katika ulimwengu wa roho ndani yake kristo.
Yohana 1:3
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika
Kila kitu kimeshafanyika mpaka majibu yako unayoyasubiri baada ya maombi, yalisha kamilika na yapo katika ulimwengu wa roho tayari.
Efeso 1:3
Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Na kwa sababu hiyo unapoomba unakuwa unatimiza utaratibu wa kuingia katika ulimwengu wa roho ili uweze kupokea majibu yako,na hii ndio sababu ni muhimu sana kuomba ukiambatanisha na neno,kwa sababu kila Baraka unayoihitaji iko ndani yake Yesu kristo(NENO ) katika ulimwengu wa roho na hivyo neno ni kama nywila ya katika benki ya majibu yako..kwa ufahamu zaidi
Kwa hiyo unapoomba maombi yako maneno huenda mbele za Mungu kama manukato(sifa) ili Mungu atoe kibali wewe kupokea majibuya maombi yako,kwa hili tunaahamu ya kuwa sifa na shukurani hufungua mageti ya mbinguni
Zaburi 100:4
Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;

Kazi hizi zote za kubeba maombi pamoja na kuleta majibu hufanywa na malaika.
Daniel 10:12
Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi. Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado

1.      Malaika  Huudumu katika kuleta ulinzi kwa Watu wa MUNGU
kuna mambo mengi yanayoendelea hapa duniani ambayo kama ukifunuliwa macho pengine huwezi kustahimili kabisa,kuna majeshi ya mapepo yanayokuwinda wewe na uhai wako usiku na mchana,kuna wachawi wanaofanya kazi ya kutafuta mlango waje kukuangamiza,kuna washirikina ambao kwa hali na mali wanashinda kwa waganga wakikuloga ili usifanikiwe,kama MUNGU asinge kuzungushia wigo wa malaika wake pengine leo ungekuwa umeangamia kabisa.
Daniel 6:21,
Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.MUNGU wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.
Kuna wakati mwingine unajikuta upo katika hatari bila wewe kujua au kujua na gafla unaona umetoka katika hiyo hatari, mpaka wewe mwenyewe unaweza ukasema umetoka kimuujiza,hii ni kwa sababu ya malaika waliotumwa kwaajili ya kuhakikisha usalama wa uhai wako.
Zaburi 34:7,
Malaika wa BWANA hufanya kituo,
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.

Ninakumbuka wakati mmoja nikiwa ninatoka chuoni mwaka 2012 pale bungeni Dodoma kuna njia panda ya rami,na nilikuwa nimepanda pikipiki(bodaboda) kuelekea nyumbani,sijui nini kilitokea lakini dereva alijikuta yuko katikati ya magari,moja lilikuwa likitoka mjini jingine likitokea njia ya uwanja wa ndege nay eye alikuwa anatokea upande wa chuo kilipo(CBE),niliona ile ajali ikitokea wakati mimi mwenyewe nikiwa nje ya barabara,sikuona aliyenirusha kutoka katika pikipiki ni nani,na nilifikaje pembeni ya barabara ninachojua ni kitu kimoja,Mungu alimtuma malaika wake ahifadhi uhai wangu.

2.      Malaika huudumu katika kuleta mavuno
Ufunuo 14:18
Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali. Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana. 19Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya MUNGU
Tumetumwa na MUNGU katika kuvuna nafsi za watu,kazi hii si rahisi kwa akili zetu wenyewe,MUNGU tayari anao malaika ili kukusaidia kuvuna hizo nafsi.wahusishe malaika katika mavuno
Wakati mwingine unaweza ukawa ni wakati wako wa mavuno(Baraka) nap engine inachelewa,mwite malaika wa mavuno akakuvunie na kukuletea
Kama wewe ni mtumishi wa Mungu kama mimi basi hapa ndio penyewe,usijaribu kufanya kila kitu mwenyewe wakati unao malaika wa kukusaidia,mwambie tu Baba atume malaika wake wakawalete watu katika ufalme wa MUNGU wakiwatokea watu katika ndoto na maono ya Usiku wakiwaelekeza mahali kanisa lilipo na kwa hakika Mungu atafanya hivyo.


3.      Malaika huudumu katika kuleta ufunuo(revelation)na ufahamu(Knowledge)
Luke 2:47,
Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.
Daniel 8:16-19
Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya.Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa.

Ufahamu juu ya neno la MUNGU na juu ya mambo yatakayo kuja badae, pia ufahamu wa mambo ya kawaida ya kila siku.
Wakati mwengine unaweza ukajikuta unashindwa kufanya kitu sio tu kwa sababu hujui jinsi ya kufanya isipokuwa unaweza ukawa umekosa ufunuo juu ya hilo jambo
Wakati mmoja nikiwa ninaomba kwaajili ya Mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zilikuwa zimepita wakati ninaomba nikasikia neno la Hekima (ufunuo juu ya jinsi ya kukabiliana na Tatizo) ya kuwa nitamke neno la kinabii juu ya huyo mama nikilenga muda na jinsia ya mtoto atakaye jifungua.nikafanya hivo,na kwa ajabu ya MUNGU siku hiyo hiyo saa nane usiku akajifungua mtoto wa kiume sawa sawa na ufunuo ulioletwa na malaika.
Unapotembea na malaika wa ufunuo mambo mengi yanakuwa rahisi sana kukabiliana nayo.

4.      Malaika hukutangulia ili Kusawazisha njia
Kutoka 23:20
Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.
Zaburi 91:11
 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake
Wakulinde katika njia zako zote.
 Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

Zaburi 91:11
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake
Wakulinde katika njia zako zote.
Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.




Malaika huudumu katika kukuletea mahitaji yako ya kimwili
1falme 19:5
Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. Malaika wa BWANA akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa MUNGU.
Umewahi kusikia pesa za miujiza?, kazi za kimiujiza,mikataba na tenda za kimiujiza? Chakula cha kimiujiza, hiini kazi ya malaika wa mahitaji, unaporuhusu awe sehemu ya maisha yako unafungua mlango wa kushangazwa kila siku na miujiza isiyo na kikomo katika maisha yako.

5.      Malaika hutia Nguvu za Kusonga Mbele
Luka 22:42
akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [ Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Kuna wakati mwengine mambo hua magumu sana kiasi kwamba unaweza ukakata tama katika imani,kama YESU alifika mahali akakata tama juu ya ile changamoto ya msalaba mbele yake,akaomba na malaika akamtia Nguvu ili asonge mbele
Unapitia wapi, kumbukaMUNGU hakutuahidi kuwa angezuia majaribu yasitupate ila alisema,ujapopita katika moto hautakugharikisha,
Unajua unapoalika malaika njia yako huwa rahisi,hukuinua na kukutia moyo,wakati watu wengine wamekukimbia Roho wa Neema huwatuma malaika kukutia nguvu na kuwa marafiki wa Karibu sana Kwako.


6.      Malaika huudumu uponyaji
Kuna malaika maalumu kwaajili ya uponyaji wako,malaika Raphael ni malaika mkuu katika mambo ya uponyaji na opereshen mbalimbali katika kuhakikisha unakuwa mzima kimwili kiakili,kiroho n.k
Yeye huusika kurejesha afya na kuweka uumbaji wa MUNGU katika ukamilifu wake, hurejesha viungo, hufanya vipofu kuona na viziwi kusikia,ni malaika kwaajili ya maisha ya afya ya mwanadamu.
Wakati mwingine unaweza ukalala ukiwa na maumivu na unashangaa unaamka asubuhi maumivu hayapo,hizo ni kazi za malaika.
Yohana 5:2
Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]



7.      Malaika huuwa(they Kill)
Pamoja na kuwa malaika hufanya kazi njema kwaajili yetu,ni kweli pia kwa wale ambao wanachezea maisha yako na kuwa kwazo mbele yako MUNGU hutuma malaika kuwaondoa kabisa,wawe ni mapepo au watu.
1 samwel 2:6
Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
Kutoka 12:29
Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.






8.      Malaika hukusindikiza kuingia katika Uzima wa milele (mbinguni)
2 falme 2:11
Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.
Luke 16:22
Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

Unapolala katika Bwana au unapochukuliwa kimaono ni malaika ndio watakuongoza kufika kule unakotarajia kufika.
Basi sasa tumeona baadhi tu ya kazi za kimalaika katika maisha yetu ni nyingi sana kiasi kwambu tukianza kutaja zinaweza kutuchukua wiki nzima kuelezea,hivo basi tuangalie aina za Malaika






AINA ZA MALAIKA
Kuna aina nyingi za malaika na wamegawanyika kulingana na majukumu yao au nafasi zao za kiutendaji.
Ikumbukwe kuwa malaika kama jeshi la ufalme wa MUNGU  wana fanya kazi katika mpango maalumu wana vyeo na ngazi za kimadaraka,na wanakwenda kwa utaratibu maalumu wa ufalme wa mbinguni.

1.      MALAIKA WAKUU
Hawa ni malaika maalumu na hutumwa kwa kazi maalumu,hawatumwi hovyohovyo(the heavenly special force) na wanapotokea jua kuna ishu nzito,na kama ni mapepo yatapata shida ni labda yafe au yaongozwe sala ya toba(mapepo hayawezi kuongozwa sala ya toba)
Malaika mmoja anauwezo wa kufanya kazi za malaika elfu na elfu,hawa ndio malaika wakuu na Jumla yao wako saba
1.      YURIEL(NURU YA MUNGU)
Huyu ni malaika ambaye anahusika sana na uangalizi wa Dunia na mahali maalumu palipowekwa kwaajili ya mateso na vifungo (Tartarus),lakini pia kulinda heshima ya Jina la Bwana wa Majeshi,kwa wale wanao tukana Jina la Bwana huyu malaika na kikosi chake ndio kazi yao
Isaya 54:17
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Unaweza ukaona kile kilichofanyika kwa kina Hauni na Miriam katika hesabu 12

2.      RAPHAEL (MUNGU mponyaji)
Huyu ni malaika aliyewekwa kwaajili ya roho za wanadamu,na uponyaji wa kila aina ya Magojwa,urejeshaji wa viungo na uhai,hufanya kazi kuhakikisha lile neno la uponyaji linakuwa halisi katika maisha yako,na unafurahia uzima wako(maandiko ya uponyaji)
3.      PHANUEL(uso wa MUNGU)
Huyu ni malaika anayehusika na Toba kwa wale wanaourithi wokovu, huusika katika kuleta majuto juu ya dhambi ili kupata toba ya Kweli na mwisho ondoleo la Dhambi.
4.      MIKAEL (nani kama Bwana)
Huyu ni malaika anaye husika katika katika maeneo makuu ya mwanadam kama uhai,lakini pia ni malaika anayehusika sana na vita na vurugu zinazosababishwa na mapepo
Ni malaika mwenye nguvu sana na anauwezo mkubwa sana wa kivita,Tunaona mara nyingi MUNGU humtumia huyu malaika katika mapambano,unaweza kuona matendo yake hapa
Ufunuo 12:7
Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.9Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa MUNGU wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za MUNGU wetu, mchana na usiku.
Yuda 1:9
Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.
5.      GABRIEL(MUNGU ni nguvu zangu)
Huyu ni malaika wa habari njema, Ndiye malaika anyetumiwa sana kuleta ufunuo na ufahamu wa mambo ya Kiroho lakini pia ni malaika ambaye MUNGU amemuweka kwaa jili ya Paradiso na uangalizi wa Kundi jingine la Malaika linaloitwa makerubi
Luka 1:19
Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za MUNGU; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema
Daniel 8:16
Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya. Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.

6.      JOPHIEL
Huyu ni malaika wa hekima na maarifa.Ni mmoja kati ya malaika wakuu ambae yuko maalumu katika kuleta neno la ufunuo neno la maarifa.
7.      SERAPHIEL
Mlaika huyu ni malaika kiongozi mkuu wa sifa za Mbinguni,ni miongoni na kiongozi wa kundi la maseraphi,aina ya malaika ambao tafsiri yake ni wanaochoma kwa moto,au malaika  wanobeba moto mkubwa. Kuchoma kwao kwa moto kunatokana na kuwa karibu sana na Mungu.






KUNDI LA PILI LA MALAIKA
MAKERUBI (wenye uhai wane)
Ufunuo 4
Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye. 8Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana MUNGU Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja. Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,
Hawa ni malaika ambao wana sura nne
I.                   Sura ya Ng’ombe – roho ya utayar,na Utumishi
II.                Sura ya Tai- uwezo wa Kuona vitu kutoka Mbali(prophetic eyes)
III.             Sura ya Simba- Ujasiri na Nguvu
IV.             Sura ya mwanadamu- upendo,utu na utashi
Malaika hawa husimama mbele ya kiti cha MUNGU, aina hii ya malaika ndio waliotumwa na MUNGU kuilinda ile njia ya mti wa uzima katika bustani ya edeni
Mwanzo 3:24
Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Lakini pia hawa ni malaika ambao MUNGU alimwamuru musa kutengeneza mfano wao ili kutitia kiti cha Rehema katika mahali patakatifu pa patakatifu na juu ya sanduku la agano.

KUNDI LA TATU
OPHANIM
Jina ophanim ni jina linalobeba maana ya wajumbe wenye magurudumu, aina hii ya malaika inafanana na magurudumu yaliyoingiliana pamoja,Ni viumbe ambao pekee wana macho kila mahali,na kazi yao ni kukibeba kiti cha MUNGU
Daniel 7:9
Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.

KUNDI LA NNE
VITI VYA ENZI (THRONES)(kigiriki THRONOROS)
Hii pia ni jamii nyingine ya malaika na aina hii ya malaika hukaa mbele za MUNGU kama wazee ishirini na nne
Colosai 1:16
Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Unapoona neno kiti cha enzi lina maana ya eneo maalumu au nafasi maalumu iliyowekwa kutawala nafasi nyingne katika ulimwengu wa roho au wa mwili,mahali palipo na kiti cha enzi pana utawala wa aina Fulani unaoamua aina Fulani ya maisha ya eneo husika.
Hawa ni malaika/wajumbe wanaohusika na utawala wa sekta mbalimbali katika ufalme wa MUNGU.


KUNDI LA TANO
MASERAFI
Neno maserafi limetokana na neno la kiebrania seraph ambalo tafsiri yake ni kuchoma, ndani ya kundi hili pia kuna aina nyingine ya malaika wakuu akiwepo malaika mkuu Michael ambaye ndiye kiongozi wa malaika wote watakatifu wa MUNGU.
Malaika hawa wa MUNGU ndio malaika wa sifa Mbinguni,na ni malaika walio karibu sana na kiti cha enzi cha Mungu na usiku na mchana hawapumziki wakilisifu jina la MUNGU wakisema mtakatifu mtakatifu mtakatifu MUNGU wa majeshi.ufunuo 4:8

MAKUNDI MENGINE YA MALAIKA
CHAYOT (ha kodesh)           - malaika watakatifu sana Ezekiel 1 na 10
ERELIM                                 –Mashujaa- isaya 33:7
HASHMALIM                       - wenye utukufu, hawani malaika ambao huonekana kama moshi hivi ni malaika ambao hutokea na kupotea Ezekiel 1:4Neno Hash-kutokea(appear) Malim- kupotea(disappear)

MALAKIM                            -Malaika wajumbe
BENE ELOHIM                    - wana wa Utukufu
ISHIM                        – Malaika wanaofanana na binadamu au wanaovaa miili ya wanadamu.












NAMNA YA KUWAVUTA MALAIKA KUWA WASHIRIKA PAMOJA NA WEWE KATIKA MAISHA YAO
1.      TENGENEZA KIU KWAAJILI YAO
Kuwa na kiu na shauku ya kutaka kufanya kazi na malaika, katika ufalme wa MUNGU kuwa na kiu na shauku hukuvuta karibu na muujiza wako,na katika mlengo huo huo unapokuwa na kiu na shauku ya kutembelewa na malaika unawavuta kuja katika maisha yako
Isaya 55:1
Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,
Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;
Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,
Bila fedha na bila thamani.

2.      TAMBUA UWEPO WAO NA MCHANGO WAO
Kuna muhubiri mmoja amewahi kusema,”kitu usichokifahamu hauwezi kukisherehekea na kitu usichokisherehekea siku moja kitaondoka katika maisha yako” maneno haya Yana ukweli Sana katika ulimwengu wa malaika.
Ufahamu wako juu ya ma,mbo ya mbinguni huvutia mbingu katika maisha yako,watu wengi wanafahamu sana kuhusu mapepo na wanajitahidi sana kujua habari zao,hii ndio sababu mapepo na ufalme wagiza huvutiwa na maisha yao.
Biblia inasema kama wakristo ni muhimu sana kuyatafakari yaliyojuu mahali kristo alipo

Wakolosai 3:2
Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.
Tuyaangalie mambo ya mbinguni na kuyatafakari hayo,fahamu zetu zijazwe na mambo ya mbinguni kila wakati,fikiri juu ya malaika,fikiri juu ya mema ambayo MUNGU amekuandalia,mambo ambayo jicho halijawahi kuyaona. Kwa namna hiyo hakika maisha yako yatajazwa na uwepo wa malaika.

3.      MALAIKA HUMTII MUNGU NA NENO LAKE
Nimeona watu wengi wakikosea sana katika hili,hutaka malaika wawatii wao,utamsikia mtu anasema,naamuru malaika waje kwako,hii ni ajabu sana na si njia ya kibiblia ya kuwafanya malaika wafanye kazi.Kumbuka malaika ni wa MUNGU na sio wa Kwako,ona YESU alivyosema juu ya malaika
Matayo 26:53
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?

Neno la msingi nami nitamsihi baba, kwahiyo basi unahitaji kumwomba MUNGU na si kuwaomba malaika, MUNGU ndiye mmiliki wa malaika
Jambo jengine ni kuwa malaika husikia sauti ya neno la MUNGU na kutii,kwa hiyo unapoomba maombi yako yote huku ukiwa umeambatanisha na neno kuwa na uhakika yakua unawavutia malaika katika kutekeleza neno ulilolitamka.
Maandiko yanasema MUNGU akituma neno lake haliwezi kumrudia bure ni lazima litatimiza kile ambacho limetumwa.
4.      KUSUDIA NA KIRI MARA KWA MARA JUU YA UWEPO WAO KWAKO.
Kama tulivyotangulia kuona malaika wanahitaji Imani ya kukiri,kili kwamba wapo hata kama huwaoni ,endelea kukiri kwa imani kwamba wapo,lazima ukiri wako uzae matunda.
Ayubu 22:28
Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako

5.      ISHI KATIKA ROHO
Malaika ni viumbe wa Kiroho wanaishi katika roho,ni muhimu kuishi katika roho ili uweze kuwa na muunganiko nao.maandiko yanasema mwili na roho vimepingana tangia mwanzo, maana yake kwa mtu wa Mwilini si rahisi na kutambua mambo ya rohoni
Kwa hiyo basi kuishi katika roho ni ufunguo wa Kwanza wa kutembea na kuishi na malaika


6.      KUWA MKALIMU(hospitality)
Tumeona moja kati ya kundi la malaika linaitwa Ishim,hawa ni malaika wanaofanana na wanadamu na wakati mwengine hutokea katika mwili,maandiko yanasema tuwe wakarimu kwa sababu wengine walipokea malaika pasipo wao kujua,
Ukarimu na upendo huwavutia sana Malaika kuliko unavyoweza kufikiri,kwa ukarimu wa Ibrahimu alipokea malaika na hivyo aliweza kumwokoa ndugu yake Lutu,lakini pia kwa kukosa ukarimu sodoma na gomora viliangamizwa kwa moto kabisa.
Amua leo kuwa mkarimu kwa wageni hasa jamii ya watu wa MUNGU.
Kwa kumaliza ni muhimu sana kufahamu ya Kuwa malaika hufanya kazi na wale watakaourithi wokovu maana yake ni lazima kuokoka kwanza,ni lazima jina lako liwe limeandikwa mbinguni.
Hivo bas ni Muhimu kuokoka na kumfanya YESU kuwa Bwana na Mwokozi wako,YESU ni neno na Neno ni YESU,Ndani yake ndimo kuna uzima ambao ni nuru yako Hapa Duniani na Mbinguni.
Ukiwa tayari kumpa Yesu maisha yako au unahitaji msaada wa Kiroho tafadhali usisite kutupigia au kutuandikia kwa namba na barua pepe zifuatazo
Namba: 0744300212/0763712031

1 comment: