MAOMBI YA UKOMBOZI MAENEO MBALIMBALI ..By prophet Kelvin raphason


REDEMPTION(KULIPIWA DENI/WOKOVU)
Kuna maneno Mawili  ya kingereza yanayoweza kutumika kwaajili ya kuelezea Neno Ukombozi,maneno haya ni Deliverance na Redemtion.Maneno haya mawili ni maneno tofauti sana lakini yanayofanya kazi pamoja,na kutokana na namna ambavyo yanamaana karibia sawa za utendaji kazi wake,si watu wengi wanaweza kutofautisha.
Tunaposema Redemtion ni neno linalotokana na Tendo redeem, ambapo tafsiri yake ni kukombolewa kutokana na Deni ulilokuwa unadaiwa, mfano tunaposema huyu amekuwa redeemed, tunamaana hapo kwanza aliwekwa rehani kwa sababu ya Deni alilokuwa akidaiwa.
Katika maandiko Neno hili linamaana ya moja kwa Moja juu ya wokovu wetu,tunasoma
Galatia 3:13
Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
katika andiko hilo hapo juu utaona neno ukombozi katika biblia ya kingereza ni redeemed,na sio delivered, hii ni kwa sababu ukombozi kwa maana ya andiko hapo juu ni kulipiwa deni.
kwa namna rahisi tunaweza tukasema hivi “Kristo alitulipia deni la torati,kwa kuwa alifanywa laana kwaajii yetu/niaba yetu”  kwa hiyo Yesu alilipa deni tuliyokuwa tunadaiwa ili tuweze kuwa wa kwake yeye,na hii ndio tafsiri hasa ya ukombozi kwa mlengo wa wokovu.
Lakini pia tunaposema hasa juu ya wokovu tunazungumzia juu ya kufanywa upya juu ya roho ya mtu, tunasoma 2cor 5:17
Mtu akiwa ndaniya kristo amekuwa kiumbe kipya,maneno haya yanamaana kubwa sana ya wokovu,neon mtu tunafahamu kuwa huzungumzia roho ya mtu na sio nafsi wala mwili kwa sababu mtu mwenyewe ni roho na anaposema ndani ya kristo ni sawa na kusema ndani ya Roho mtakatifu anafanyika kuwa kiumbe kipya ya kale yaani ule utu wa kale ambao ulikuwa ndani ya mauti na dhambi unafanywa upya kwa kule kuwa ndani ya Roho Mtakatifu,na huu ndio ubatizo wa Roho mtakatifu(Rejea kitabu cha Viwango vya Roho Mtakatifu).
Sasa kumbuka mtu si roho pekee,bali anayo nyumba inayoitwa mwili na iliyopewa nafsi(akili,utashi na moyo) na kwa sababu hiyo unaposhughulikia oho yako kwa kuupokea wokovu ni lazima pia utiishe mwili wako ili kufanya mapenzi ya MUNGU,hii ni kwa sababu mwili kwaasili hauwezi kuokoka biblia inasema
(mwili ni wa mauti)
Asili ya mwili ni chini na ni mauti wakati roho yako asili yake ni ya juu.katika kuutiisha mwili ni Pamoja na kuvifisha viungo na kufungua vifungo vilivyofunga nafsi yako na mwili wako ili mwili na nafsi yako isiwe kikwazo kwa roho yako katika kutenda mapenzi ya Mungu. Hii ndio sababu utaona Biblia inasema mwili unapokuwa na Nguvu hupingana na roho yako na kwasababu hiyo hutaweza kufanya mapenzi ya Mungu kikamilifu.
Galatia 5
Mfano: jaribu kufikiri unaweza ukawa unatamani sana kwenda kanisani na umeamka asubuhi unakuta mwili wako ni mgonjwa wote,je utakwenda? Au unajua wapo watu ambao wanatamani sana kuomba lakini kila wakijaribu kuomba wanasikia uchovu gafla na wanajikuta wanakosa hamui ya kufanya maombi,Je unadhani hiyo ni hali ya kawaida? Ni vifungo vilivyoko katika mwili ambavyo visiposhughulikiwa vinazuia roho yako kufanya mapenzi ya MUNGU. Na hapo ndipo inapohitajika kufanya ukombozi yaani deliverance ili kupokea uhuru kamili.

DELIVERANCE
Tunapozungumza juu ya deliverance hatugusi juu ya kazi ya Yesu ya msalaba kwa maana ya kulipiwa deni (redemption) kwa kuwa deliverance ni tendo linalofuata baada ya redemption. Na kama tulivyotangulia kuangalia hapo mwanzoni kuwa ni roho ndio hupokea wokovu,kwa namna nyingine naweza kukwambia kuwa roho yako haiitajio deliverance inahitaji redempition kwa sababu unapompokea Yesu kristo Yeye mwenyewe kwa damu yake anatufanya kuwa wapya katika roho. Kinachotokea baada ya kufanywa upya kwa roho yako unahitaji kuanza kushughulikia vifungo vilivyoko ndani ya nafsi na mwili wako ili kuleta wepesi wa roho yako kufanya mapenzi ya Mungu. Ili kuelewa zaidi tuangalie mfano huu uliopo ndani ya Neno la MUNGU.
yohana 11:43
Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44Akatoka nje yule aliyekufa, akiwa amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
kwa Mfano huu tunaweza kuelewa uhusiano kati ya ukombozi(redemption) na ukombozi(deliverance)
katika maandiko yaliyopo hapo juu utaona matukio yaliyotokea na kufuatana katika kumfufua lazalo na nitajaribu kuainisha kila kipengere cha tukio ili uweze kuelewa zaidi.
a.      Liondoeni Jiwe
Lazaro ni mfano wa mtu aliyekatika dhambi,ambaye hajaokoka wala hamjui yesu,mtu wa aina hii maandiko yanaweka wazi ya kwamba anajina la kuwa hai lakini anakuwa amekufa roho yake(ametengwa na Mungu)
ufunuo 3:1
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
sasa mtu huyu roho yake inapotengana na Mungu mapepo huweka kifuniko juu yake ambalo ni mfano wa jiwe katika kaburi la Lazaro ili kusudi asisikie injili ya kristo asije akafufuka na hata akifufuka ashindwe kutoka nje.
Hiii ndio sababu  Yesu anaagiza “liondoeni jiwe” maana yake fanyeni maombi yatakayotengeneza mazingira ya kifuniko juu ya watu wenye dhambi kuondolewa. Ikumbukwe kuwa Mungu hafanyi kitu duniani isipokuwa mtu mmoja ametengeneza nguvu ndani yake ili azitumie kufanya mambo makubwa,na nguvu hii hutengenezwa kwa njia ya maombi.
kwa hiyo kama watu wasipoomba juu ya eneo wanalotaka watu waokoke,wanaweza kushangaa wanahubiri sana na watu hawaokoki au wanaokoka lakini wanarudi dhambini, hii ni kwasababu wanakuwa na kifuniko bado juu ya maisha yao.
b.      Yesu akamwita lazaro Toka nje
Sasa hii ni hatua ya pili baada ya kuondoa jiwe Yesu anamwita lazaro (mwenye dhambi) aje katika wokovu, tukumbuke kuwa anayeokoa ni Yesu kristo na si mwanamaombi. sasa katika hatua hii Yesu anamwita lazaro atoke nje,awe hai, na lazaro anatoka,huu ni mfano wa ukombozi kwa maana ya redemption.
c.       Mfungueni sanda mkamwache aende zake
katika hatua hii Yesu anaagiza Yule aliyetoka kaburini na sanda afunguliwe sanda ili awe huru kabisa,huu ni mfano wa ukombozi kwa maanda ya deliverance,ya kwamba mtu anaweza akawa ameokoka (amefufuka) na ametoka kaburini lakini bado yuko chini ya vifungo (sanda) vitakavyomfanya pamoja na kuwa amepokea uzima wa milele ndani yake,kuna vifungo katika mwili wake na nafsi yake vinaweza vikamfanya akapoteza uzima wake.
Redemtion hushughurika na roho yako na deliverance hushughulika na mwili wako.
1cor 5:7
Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
unaweza ukawa umeokoka lakini kwa sababu ya chachu ndogo katika mwili wako ukashindwa kuuona wema wa Mungu katika maisha yako.
hivyo basi Deliverance ni jumla ya maombi yanayomfungua Mtu kutoka katika sanda au chachu ili afurahie uhuru wake ndani ya Kristo Yesu
Kitabu hiki kipo kwaajili ya kukusaidia kuiona chachu na sanda mbalimbali katika vipengera tofauti ili uweze kuomba na hatimaye kufunguliwa kabisa vifungo,unaposoma kitabu hiki ni maombi yangu kuwa  Roho wa Mungu akuwezeshe kuona zaidi ya kile kilichomo ndani ya kitabu hiki ili uweze kupokea uhuru kamili katika Jina la Yesu.





MAELEZO MUHIMU
Ndani ya kitabu hiki utakuta vipengere mbalimbali vinavyoelezea aina ya jambo linalohitaji kufunguliwa pamoja na Maelekezo ya namna ya Kuweza kuomba.
hivyo basi Fuata maelekezo hayo kwa usahihi ili kuweza kupoke kile unachoomba,kama nyumbani kwako hauna mafuta ya ukombozi/unaweza ukayapata kwa kuja kanisani au ukatumia mafuta yoyote ambayo umekwisha kuyaombea kama kipitishaji cha upako wa Roho Mtakatifu(Channel of Anointing).




















MAOMBI YA UKOMBOZI
1.      KATAA KUWA SEHEMU YA MAISHA YALIYOPITA
kuna watu wengi wanaishi maisha ambayo siyo ya kwao,na wanajaribu kujinasua na kutoka katia maisha hayo lakini kwao inakuwa sio rahisi,kulingana na hali waliyonayo na mazingira yanayowazunguka kila siku. Wewe unaweza ukawa ni mmoja kati ya watu wa namna hiyo, ambao watakalo kulifanya hawafanyi lakini wanafanya wasilo litaka.
warumi 7:15
Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda”
Usijilaumu juu ya kile unachokipitia,kwa sababu inawezekana si makosa yako mpaka umefika hapo,labda unaweza ukawa unapitia kile kile ambacho Mtume Paulo anakizungumza katika mistari hiyo tuliyoipitia,au labda wewe ni matokeo yanayofanana na hali ya mafarisayo wakati wa Yesu
mathayo 23:29
Ole wenu, Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya Jehanamu? Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.
kitu kimoja ambacho si watu wengi wanakijua ni kuwa,sheria ya uumbaji inafanya kila kitu kuzaa kitu kinachofanana nacho yaani kila kitu hujizidisha katika namna ile ile ambayo iliumbwa tangia mwanzo
 mwanzo 1:29
Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mmea utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa chakula chenu”
mfano ni kama hilo andiko hapo juu,unaona Mungu anaumba Matunda ambayo ndani yake yanambegu za kuzalisha matunda ya aina ileile ambayo imetoka,mchungwa kuzaa mchungwa,mpera huzaa mpera,mtu huzaa Mtu,na mnyama huzaa aina ileile ya mnyama,hiyo ndio sheria(order) ya uumbaji.
Kwa kule kusema aina ilele ya uumbaji ninamaana kila mbegu ndani yake hubeba vinasaba(genes) ambavyo ndani yake vimebeba tabia,na alama za ukoo.
mwanzo 49:3
Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,
Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu.
Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.

unaona reubeni kama mzaliwa wa kwanza amebeba nguvu ama uwezo wa yakobo na kama yakobo alivyowapita wengine vile vile na reubeni. sasa ukiangalia mistari ile ya mathayo 23,utaona ile oda ya uumbaji ikiendelea kwa mafarisayo.
pamoja na kuwa mafarisayo hawakupenda yale ambayo baba zao waliyafanya,hawakuwa na namna ya kujiepusha nayo kwa sababu yalikuwa ndani ya damu yao na walikuwa tayari wameanza kuyafanya bila kujua,Baba zao waliwauwa manabii na wenye haki huku watakatifu wengine wakiwafukuza mji kwa mji,na hapa bila kujua walikuwa wakipanga njama za kumuuwa Yesu,hiyo ilikuwa katika damu zao na isingeweza kuepukika kirahisi,kwa sababu wao walikuwa ni malimbuko na uwezo wa wazazi wao.
wakati mwengine unaweza ukajikuta kile ambacho ndani ya roho yako unatamani sicho unachokifanya,unajikuta unapitia yale yale ambayo baba zako waliyapitia,inawezekana unapitia umasikini ule ule ambao baba zako waliupitia,magonjwa yale yale ambayo baba zako waliumwa,na shida zile zile.kama walizo pitia wazazi wako. hiyo inaitwa laana ya vizazi (generation curse)
lakini habari njema ni hii siku ulipookoka Mungu aalikupandikiza katika ukoo wa ibrahimu,isaka na Israel wagalatia 3:14,hivyo unapokea haki kwa hiyari yako kujinasua katika laana ambayo ilikuwa juu ya wazazi wako,mababu zako na wahenga wako wote,unahaki ya kuchagua kuishi maisha yako na si maisha yao.
pamoja na kuwa wewe hukupanga uwe kama ulivyo,na hali hiyo inakusumbua na unatamani kuachana nayo lakini unashindwa,hii ni kwasababu wewe umebeba aina ile ile ya wazazi (genes) na hivyo ili uweze kutoka katika uharibifu huo unahitaji aina nyingine ya vinasaba,Tunasoma
Galatia 3:13-14
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14ili kwamba baraka ya Abrahamu iwafikie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani”
Laana ya torati ni laana ya sheria,ni matokeo ya sheria inapovunjwa au kuharibiwa au kutofuatwa,sasa kama sheria ya uumbaji ilitaka watu wafanane na Mungu mwanzo 1:26,lakini wakachagua kuvunja sheria na kutaka kufanana na adui,laana ambayo ni kisasi cha sheria huingia kwenye mifumo yao.
labda nijaribu namna hii,ikiwa neno la Mungu ndio sheria Njema ya uumbaji,na sheria hii ilisema,Na tumfanye Mtu kwa sura(roho) na mfano(nafsi) wetu mwanzo 1:26,maana yake lile neno jema yaani sheria lilikaa nda ni ya nafsi ya Mtu na roho ya Mtu na kuleta mtiririko wa vinasaba vya kiungu (genes) katika nafsi na roho ya Mtu na kumfanya awe nafsi hai,ni hivyo kufanya kila kilichozaliwa kwa Yule mtu wa kwanza kuwa na aina ya uungu na uhai.
halafu kisha Yule mtu aliyepokea ile sheria ya uzima akaamua kusikia neno la Mauti kutoka kwa shetani kwa hiari yake,maana yake ni kuwa alichagua mtiririko mwingine wa vinasaba ndani ya nafsi yake na roho yake ambavyo,badala ya kuleta Uzima ndani yake vilileta mauti na japokuwa mtu alibaki na sura na mfano wa Mungu mtiririko wa uhai ulibadilishwa na kuwa mauti,na kulingana na sheria ya uumbaji kama tulivyoona mwanzo 1:29,kila mtu aliipokea mauti hata kama hakutaka.ona.
warumi 5:12
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi
hivyo inapotokea babu zako baada ya adamu waliingia katika mikataba mbalimbali ya kishetani kama matambiko,uganga,uchawi ili kupata msaada wa kipepo,au walimwaga damu ya mtu asiye na hatia ili kupata mali kwa nguvu au kulipiza kisasi,waliaribu pia mtiririko wa vinasaba vya uumbaji,kwa hiyo hata kama haukutaka kuwa hivyo utakuwa kwa sababu ya kilichopo ndani ya Damu yako
lakini Habari njema ni Kuwa kifo cha yesu kilivunja hiyo sheria  na kutuunganisha na mtiririko ulio bora zaidi,ya ule wa kwanza kwa hiyari yetu. unapokubali na kumwamiini Yesu Kristo,unahamishwa kutoka katika mtiririko wa mauti na kuingia katika mtiririko wa uzima,na kuanzia kwako kila utakacho zaa kitakuwa na uzima.
NAMNA YA KUVUNJA MTIRIRIKO NA VINASABA VYA MABABU ZAKO NA KUPOKEA VINASABA VIPYA KATIKA MAISHA YAKO.(DELIVERANCE FROM GENERATION CURSE)
1.      NI LAZIMA UOKOKE
Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu
Kuokoka ni hatua ya kwanza inayokufungua kutoka katika vifungo vya dhambi ya Adamu,na kukupa haki na neema ya kutoka katika vifungo vingine kwa hiyari yako mwenyewe.
ili kuuona ufalme wa Mungu(yaani kuwa na utawala wa Mungu katika maisha yako) kuzaliwa mara ya pili(kuokoka) ni lazima.
Yohana 3:3
Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
2.      OMBA  MAOMBI YA KUJITENGA NA LAANA ZA VIZAZI
ikiwa Babu zako au wewe mwenyewe uliingia katika mikataba ya kishetani ili kupata msaada,ili kutoka utahitaji wewe mwenyewe kujitoa kupitia damu ya Yesu. Damu ya yesu ipo kwaajili ya kukusaidia utoke katika hiyo mikataba ya kipepo utakapoamua kutoka.
ufunuo 12:11
“Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”
mwisho wa somo hili utaona kuna maombi ya ukombozi(prayer point) anza kuomba hizo na utaona Mungu akikufungua na kukuweka huru,bila shaka pia unaweza ukahudhuria katika ibada zetu za maombi ya ukombozi kila alhamisi na Jumapili katika Makanisa yetu ya URU(ubalozi wa Roho wa Uzima) Ministries
3.      KULA MWILI NA DAMU YA YESU
Mwili na Damu ya Yesu ni siraha lakini pia ni vifaa vya kiungu kwaajili ya kukupandikiza katika uzao wa kiungu
yohana 6:56
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. 58Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele
Mwili wa Yesu katika umbo la Mkate na Damu ya Yesu katika umbo la Divai hufanya mtu kuunganishwa katika uzao na mtiririko wa vinasaba vya kiungu na hivyo kupokea uhai kutoka kwa Mungu, Yesu anasema  mababa walikula chakula ambacho si mwili na damu ya Yesu nao wakafa au kwa tafsiri nyingine wakaleta mauti,Yeye atakaye mla yeye atapokea tena mtiririko wa uzima ndani yake.
unapokula mwili wa Yesu unapokea Baraka zitokanazo na kazi ya Yesu ya msalaba ambazo ni uponyaji kutoka katika magonjwa ya aina zote, isaya 53:5, unafunguliwa kutoka katika umasikini wote 2corth 8:9 na pia unapokea kuhuishwa upya.
unapokunywa damu ya Yesu unaingiza vinasaba(genes) ndani ya nafsi yako na Damu yako na hivyo kupokea Mbegu na aina ya mbinguni,na kama kuna agano lolote huvunjwa kwa hiyo damu ya Yesu. kwa kule kunywa Damu ya Yesu kila magonjwa ndani ya damu na nafsi huharibiwa kabisa.

4.      SOMA NENO LA MUNGU NA KULIISHI
Neno la Mungu huleta virutubisho vya uzima ulioupokea na kwa kadili unavyozidi kusoma na kuishi ndani ya Neno, Ule utu upya ulioupokea huuwishwa kila siku na kukua hata kufikia mtu mkamilifu.
Yohana 1:1-5
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; nwala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.

.
MAOMBI YA UKOMBOZI
1.      Baba katika jina la Yesu ninatubu kwa makosa na dhambi na uovu uliofanywa na wahenga wangu ambao umeletwa juu yangu na uzao wangu,ninamwaga Damu ya yesu katika malango ya kuzaliwa kwangu na ndani yangu katika jina la Yesu
2.      Ninajitenga na kila laana za mababu na mabibi zilizoko juu ya maisha yangu,ninakata kila mti wa laana za kurithi kutoka kwa mababu na mabibi,na ninajipandikiza katika uzao wa Yesu kriso ambao ni uzao wa Ibrahimu.
3.      Ninarudisha mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/mababa ,katika Jina la Yesu.
4.      Nina zilaani roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano katika maisha yangu na naziamuru kuniachia kwa Jina la Yesu[ Sema mara 3 na anza kusema hivi,”niachie kwa jina la Yesu
5.      kila roho simamizi zinazo zidi kutilia mkazo umiliki wake juu yangu ziteketee kwa Moto wa Roho mtakatifu katika Jina la Yesu Kristo.
6.      ninatangaza kuwa mimi si sehemu ya uovu wao,Damu yao,Laana zao. mimi ni mzao wa Ibrahimu,ukuhani wa Kifalme taifa takatifu tu wa milki ya Mungu.
maelekezo ya kinabii:
Chukua mwili na Damu ya Yesu kisha kula na Kunywa,kisha tangaza uhuru wako kutoka katika laana ya Vizazi





KUFUNGULIWA NIRA
Kwa wale walioko vijijini au umewahi kuona maisha ya mashambani huko vijijini unaweza ukaelewa pale biblia inapozungumza juu ya Nira.
nira ni kifaa kilichotengenezwa kwa Miti na miti hii hufungwa shingoni mwa ngombe,lengo hasa ni ili kumsaidia mkulima kuwaongoza ng’ombe vema wakati wa kulima,nira inapofungwa juu ya ng’ombe au punda,unaweza kumwongoza mahali popote unapohitaji aende,utambebesha mizigo na kumwongoza apeleke mahali popote.

katika ulimwengu wa roho kuna mfumo unaofanana na huo katika ulimwengu wa giza,mapepo yanapotaka kumwongoza mtu mahali yanapotaka humfunga kwanza huyo mtu ndani ya nira,na kisha humtwisha mizigo na kumpeleka mahali popote yanapohitaji aende.tofauti yake huwa nira hizi huwa sio miti isipokuwa aina Fulani ya roho,zinapandikizwa katika maisha yako ili kukufanya ufanye vitu bila wewe kutaka.
Mfano mzuri wa roho hizi ni Roho za madeni,ulevi,uzinzi n.k
kwa kupandikiza roho hizi mtu hatakuwa na maamuzi juu ya mapato yake anayoyapata na maisha yake,hii ndio sababu unaweza ukakuta mtu anapata fedha halafu yote inaishia baa,inaishia kwenye madeni,au kulipia bili za hispitali.
Chini ya roho hizi mtu hataweza kufanya maendeleo yeyote,mtume na Nabii Paulo anasema

warumi 7:15
Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia

unaweza ukawa hupendi kwa hakika kile unachokifanya,lakini unajikuta unafanya hata kama hupendi,unajaribu kuacha lakini badala ya kuacha unajikuta ndio kwanza umechochea,ni kwa sababu umefungwa nira na hautaweza kutoka hapo mpaka Yesu Kristo akufungue.
mara nyingi roho hizi  huingia ndani ya mtu pale Mtu anapofungua mlango wa haya mapepo kuingia,kwa faida nitakwenda kukuonesha milango hiyo ya kipepo ili usiwe muhanga tena wa kuvikwa nira.

1.      Dhambi
huu ni mlango mkubwa wa Mapepo kuingia ndani ya Mtu,maandiko yanasema
1yohana 3:8
Yatendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

2.      Kupitia kupokea au kuona vitu vilivyolaaniwa(cursed materials)
huu ni mlango wa pili wa ambao shetani huutumia ili kuingiza roho za uharibifu katika maisha yako,kila kitu kinachoonekana kina uwezo wa kubeba roho kwa sababu kina mwili,na kwa sababu hiyo ni rahisi kwa vitu kuweza kutumiwa na shetani katika kubeba roho zitakazo haribu maisha yako,sio watu wengi wanajua ya kwamba hata tu kwa kule kuona vitu vilivyobeba roho unaweza kupokea hiyo roho chafu
ayubu 31
Nilifanya agano na macho yangu;
Basi ningewezaje kumwangalia msichana?

macho ni mlango wa moyo na mwili,kwa sababu kwa kuona mtu hupokea imani na imani
ni roho,hivyo hivyo kupitia kuona unaweza ukapokea roho za uasherati,ulevi,uasi n.k
dawa ya kutokuvamiwa na roho zinazowinda macho yako ni kupitia kuweka agano na macho yako lakini pia,hii ndio sababu unaona mtume Paulo anasisitiza juu ya kutakasa vitu kwa neno na kuomba.
1timotheo 4:5
“kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”   
Angalia mstari huu
zaburi 119:91
Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,
Maana vitu vyote ni watumishi wako.

kwa kule kusema vitu vyote ni watumishi wako,ina maana vitu vinaweza kutumika katika kutekeleza makusudi Fulani,unapokomboa kitu chochote kwa maombi na kwa neno unaviweka kuwa chini ya Mungu kwaajili ya Utumishi,lakini usipovikomboa vinaweza kutumika na shetani ili kubeba roho za uharibifu na hivyo kukufunga katika maisha yako.fikiria kama magari yangekuwa watumishi wa Mungu ajali zingetoka wapi!.
3.      Ndoto.
Ndoto pia ni mlango wa adui,hasa inapotokea mtu amelala bila kuwa na ulinzi wa Mungu,unapoomba wakati wa kulala unaruhusu Mungu kutawala mipaka na malango ya roho yako na nafsi yako na hivyo kumfanya shetani kukosa mlango wa kuingia na kuharibu.
matayo 13:25
“lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake”
unaona watu walinapolala bila ulinzi wa Mungu shetani huja na kupandikiza roho za uharibifu ndani ya maisha yao kwa njia ya ndoto,mfano wa ndoto ambazo hudhihirisha uvamizi wa adui ni kama mtu anapoota anakula vyakula hasa nyama asizozijua,kuota unakimbizwa na nyoka,kuota unafanya tendo la ndoa na mtu unayemfahamu au usiyemfahamu n.k
hii ndio sababu imeandikwa
zaburi 127:1
BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wanafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye anakesha bure.
             hakikisha unapoamua kulala,unapata muda wa kuomba na kutafakari neno la Mungu.
kama umekuwa muhanga wa maeneo hayo na hata ambayo sijayataja usiogope,habari njema nikuwa

isaya 10:27
Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.

siku ya leo nisiku ambayo kila nira juu ya maisha yako inakwenda kuvunjwa,na kila mzigo(majukumu) ambayo shetani amekutwisha mabegani mwako yataharibiwa kwa damu ya Yesu.
Mungu anakwenda kuku weka huru Muda Mfupi ujao,utakapoamua kufuata maombi haya ya kinabii,hii imehakikisha.

maelekezo ya kinabii:
Chukua mafuta ya Ukmbozi (oil of Deliverance) kisha paka    kichwani kwako na shingoni mwako kisha anza kuomba maombi haya.

1.      Baba katika jina la Yesu kila nira ambayo shetani ameiweka katika maisha yangu,iharibiwe sasa kwa mafuta haya.
2.      kila mzigo wa majukumu ambao shetani amenitwishwa ili kunifanya masikini,mnyonge na dhaifu ninauondoa sasa katika jina la Yesu.
3.      kila wachungaji wa kipepo wanaolazimisha bado nia kubaki kwenye maisha yangu waharibiwe kabisa na kuwa majivu katika jina la Yesu
4.      ninatangaza uhuru wangu,kutoka katika katika kila nira za magonjwa,umasikini,madeni n.k(taja)
5.      ninatangaza kuwa mimi ni mwali wa Moto na hakuna silaha itakayofanyika juu yangu itafanikiwa katika jina la Yesu Kristo.

3.  KUSHUGHULIKIA ROHO YA HOFU YA KIPEPO.
kuna aina mbili za hofu ambazo zimatajwa katika biblia
1.      hofu ya Mungu
2.      Hofu ya kipepo
HOFU YA MUNGU
hofu ya Mungu,biblia inasema ndio uchaji,yaani kumcha Mungu na kuchukia uovu,ni kutetemeka unaposikia neno la Mungu,isaya 66:2
hofu ya aina hii huletwa na Roho mtakatifu na ni moja kati ya roho saba za Mungu zilizoachiliwa kwa watoto wa Mungu isaya 11.
HOFU YA KIPEPO
aina ya pili ya hofu ndiyo nataka twende tukaishughulikie siku ya leo,ni hofu ya kishetani au hofu ya kipepo,Aina hii ya hofu ndio mlango Mkubwa wa shetani anapotaka kuharibu maisha yako,mara nyingi kabla shetani hajaharibu maisha ya mtu,hutafuta mlango wa kuingia katika eneo la Maisha yako,na moja kati ya vitu ambavyo anatumia ni vitisho vinavyotengeneza mlango wa hofu, na kisha akishapata mlango huingia ndani na kufanya uharibifu.
hii ndio sababu utaona katika neno la Mungu,mara nyingi Mungu anapotuma malaika au Yesu kristo anapowatokea wanafunzi wake huanza na neno “Usiogope” kwa sababu ukiogopa mlango wa mapepo hufunguliwa na hivyo kumzuia Mungu kufanya kazi.
dada yangu na kaka yangu,hofu ni roho inayotoka kuzimu,haitokani na Mungu,hofu ya aina yoyote,hofu ya usiku yaani huwezi kulala peke yako,bila taa,huwezi kupita makaburini,hofu ya wachawi,hofu ya magonjwa,hofu ya umasikini,hofu juu ya mambo ya baadae,hofu ya talaka,hofu ya kushindwa,zote na nyinginezo,hazitokani na Mungu,ndio maana maandiko yanasema
2timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga,(hofu) bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
unaporuhusu roho ya hofu tu ndani yako ndipo uharibifu hutokea,roho ya hofu huzuia uwepo wa Mungu katika maisha yako
waebrania 10:38
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.

pindi tu unapookoka unaitwa mwenye haki wa Mungu,na mategemeo ya Baba Mungu ni kuwa uishi maisha ya imani kinyume na hofu,mwenye haki anapoanza kuruhusu hofu za kipepo katika maisha yake humfanya Mungu kuhuzunika na kutokuwa na furaha naye.
siku ya Leo ninakemea roho ya hofu ndani yako ikuache mara moja katika Jina la Yesu kristo,karibu sasa tuanze kuomba.
maelekezo ya kinabii: Chukua mafuta ya ukombozi,na kisha Jipake katika kichwa chako na uombe maombi haya.
Maombi.
1.      katika Jina la Yesu Kristo,ninaharibu kila milango ya hofu katika Maisha yangu kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo
2.      Ninag’oa kila mapando na visababishi vya roho ya hofu katika maisha yangu Katika Jina la Yesu
3.      ninakataa kuwa mtumwa wa Hofu na mashaka ya aina yoyote,hofu ya usiku,hofu ya kifedha(taja aina ya hofu inayokusumbua) katika jina la Yesu.
4.      roho mtakatifu,Nipatie roho ya Nguvu na ya moyo wa Kiasi katika Jina la Yesu














 UKOMBOZI WA MIGUU
Ni muhimu sana kufanya ukombozi wa Miguu mara kwa mara hii ni kwasababu ya umuhimu wa miguu katika mafanikio ya Mtu binafsi na hata maeneo husika.Katika maandiko Miguu ni eneo linaloanzia katika maungio ya kiuno mpaka chini kabisa ya nyayo za Mtu, eneo hili hasa nyayo ni maeneo Muhimu sana ya kuyaangalia unapofanya Maombi ya Ukombozi, sasa hebu tuangalie Jinsi gani Miguu inaumuhimu katika umiliki wa maisha ya Mtu
1.      Miguu ni malango ya kumiliki
Yoshua 1:3-4
Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, Kama nilivyomwapia Musa.
Angalia mahali mtakapokanyaga miguu yenu nimewapa,kwa tafsiri nyingine Mungu anajaribu kusema ninatumia nyayo zenu kupitisha umiliki katika maisha yenu.
hii ndio sababu ni muhimu sana kulinda mahali nyayo zako zinakanyaga kwa sababu mahali utakapokanyaga utapamiliki,unaweza usimiliki katika ulimwengu wa mwili lakini katika ulimwengu wa roho unapokanyaga mahali kama mtu wa Mungu nyayo zako zanaanza kumiliki kila kilichopo katika hilo eneo.
Kuna watu wengi wana matatizo ya Miguu,hii ni kwasababu anaweza akawa ametembea katika eneo ambalo ardhi yake inamatatizo,labda ni ardhi iliyobeba ushirikina au laana au magojwa,na kwa sababu namna Mungu alivyoumba miguu yako ni kwaajili ya kumiliki,unajikuta kwa kule kukanyaga katika ardhi ya namna hiyo unamiliki  pamoja na magonjwa,laana na uchawi .hii ndio sababu unahitaji kufanya maombi ya ukombozi mara kwa mara wa miguu yako.
Mungu alipoilaani ardhi katika mwanzo 3:17  maisha ya adamu yalikuwa ni magumu,hii ni kwasababu miguu yake ilimiliki laana iliyokuwa katika ardhi.
habari njema ni kuwa Leo unakwenda kufunguliwa katika jina la Yesu.
maelekezo ya kinabii: chukua maji katika Beseni yaombee yawe Damu ya yesu,  halafu nawa nyayo zako za miguu,Baada ya maombi haya chini.
Maombi:
-          Baba kwa damu ya thamani ya Yesu kristo,ninaomba utakaso wa Miguu yangu,nyayo zangu katika jina la Yesu
-          Kila kitu kilichopenyezwa Na Adui katika nyayo zangu kupitia ardhi kiharibiwe sasa katika jina la Yesu
ukiwa unaomba ombi hili anza kuosha miguu yako,au kama upo na familia kuhani wa familia afanye hiyo kazi na kisha ajioshe mwenyewe.
-          ninatakasa kwa damu ya Yesu lango langu la umiliki kwa miguu na kupitia Damu Yesu ,kila sumu iliyoko katika miguu yangu iharibiwe kabisa katika Jina la Yesu.


2.Miguu kama silaha

efeso 6:15
“na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
Luka 10:19
“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Mungu anatuonesha jambo hapa ya kuwa kupitia miguu unaweza kujipatia ushindi kamili katika maisha yako
Mamlaka ya kukanyaga sio kushika ni kukanyaga kwa nyayo zako mamlaka za shetani,hii ni kukuonesha kuwa kupitia miguu yako Mungu anaweza kuudhibiti utawala wa shetani katika maisha yako.
Mwanzo 3:15
“nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
ni mpango wa Mungu kutumia miguu yako katika kuleta ushindi kwako na katika ufalme wake,hii ndio sababu shetani nae hali akijua ya kuwa Mungu ameachilia uwezo wa kivita katika miguu yako,haachi kuhakikisha anaharibu hiyo asili ya uwezo wako
watu wengi katika ulimwengu wa roho miguu wanayotembelea sio ya kwao,wengine miguu yao imebadilishwa na wamevikwa miguu ya aina nyingine,wengini miguu yao imechukuliwa mateka ndio sababu hawawezi tena kuitumia miguu yao kwaajili ya kumiliki ,
DALILI ZA MIGUU ILIYOCHINI YA UVAMIZI
1.      kukosa nguvu
2.      kuuma mara kwa mara hasa katika nyayo
3.      kuumwa kichwa mara kwa mara
4.      kuota ndoto unakimbizwa na huwezi kukimbia
5.      kuota umekanyaga peku chooni au unakanyaga miiba
6.      kuvimba miguu
 Maelekezo ya kinabii: Chukua maji katika beseni changanya na damu ya Yesu,kisha loweka miguu yako ndani na omba maombi haya kwa imani.
1.      Baba kwa damu yako ya thamani ninaomba rehema kwa kuruhusu adui kunyanganya mamlaka iliyoko katika miguu yangu.
2.      kwa damu ya Thamani  ninaikomboa miguu yangu mahali popote ilipofungwa,kutekwa au kuibiwa katika Jina la Yesu
3.      ninatuma Moto na radi katika magereza yote ya kiroho mahali ambapo miguu yangu imefungiwa
4.      ninaharibu kila mapepo yaliyoko katika miguu yangu kwa damu ya Yesu,kila pando lililopandwa katika miguu yangu na nyayo zangu ambalo baba hajalipanda ling’olewe sasa katika jina la Yesu.
5.      ninatangaza chini ya upako wa Roho mtakatifu ya kuwa niko huru kabisa.























UKOMBOZI KUTOKA KATIKA VIFUNGO VYA NAFSI
Nafsi ni eneo ambalo lipo kati ya mwili wa Mtu na roho ya mtu,nafsi ninahusisha maeneo matatu muhimu katika kumfanya mtu kuwa hai,ambayo ni akili,utashi na Moyo
Akili: ndio mahali yanapofanyika maamuzi na majadiliano kwaajili ya hatima ya maeneo mengine ya Mtu, akili ya mtu inapokuwa ni njema na maisha yake huwa mazuri
utashi:,ni mahali ambapo ndipo haiba ya mtu hupatikana ikiwamo tabia,na ule uwezo wa kujitambua kuwa wewe ni nani na nini unahitaji kufanya,lakini pia hapa ndio mahali mtu hutofautishwa na mnyama.
Moyo: ndipo mahali vinapohivaziwa vitu vyote vinavyoingia kupitia milango ya fahamu,hii ndio sababu maandiko yanasema linda sana moyo wako kuliko vyote uvilindavyo kwa kuwa humo kunatoka chemichemi ya uzima
mathayo 15:19
Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
sasa nafsi ya mtu inaweza kufungwa,au kuibiwa au kuharibiwa kwa sababu shetani anaamri juu ya mwili wako na nafsi yako lakini hana amri ya roho yako. Nafsi ya mtu inaweza kushambuliwa na mapepo katika mazingira ya aina tatu
1.      mapepo yanaweza kumshambulia mtu yakiwa ndani yake
2.      mapepo yanaweza kumshambulia mtu yakiwa nje ya Mtu
3.      mapepo yanaweza kumshambulia mtu yakiwa yameambatanishwa au kushikishwa na nafsi ya Mtu.


1.      MAPEPO NDANI YA NAFSI YA MTU.
mapepo yanapokuwa ndani ya nafsi ya mtu yanakuwa yanaendesha shughuli zote zinazohusu nafsi,yaani akili yake inakuwa na mapepo na mtu huyu hataweza kabisa kufikiri kwa kutumia akili yake aliyopewa na Mungu,hapa ndo unaona mtu alikuwa na akili sana mara gafla akili yake imepotea dalasani, mtu huyu hata weza kuwa na utashi ambao aliumbiwa,namna ya haiba yake huingiliwa na adui,ndio sababu utaona hata jinsi anavyoonesha tabia yake ni ajabu ajabu,pia mtu ambaye ndani ya nafsi yake kuna mapepo,utaona ya kuwa hata mawazo yaliyoko ndani ya moyo wake ni mabaya tu,na kinachohifadhiwa ndani yake si  chema
unapokutana na Mtu wa namna hii unajua tu ya kuwa ndani ya nafsi yake kumetawaliwa na mapepo.
mfano:marko 5:1
Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerase. 2Na alipokwisha kushuka katika mashua, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; 3makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu yeyote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe

2.      MAPEPO NDANI YANAYOSHAMBULIA KUTOKEA NJE YA NAFSI YA MTU
kuna mtu mwingine ndani yake hakuna mapepo lakini napepo yanakua yanamshambulia kwa nje ya nafsi yake,mtu huyu maisha yake huwa ni ya kubadilika badilika,kuna wakati anakuwa na akili,kuna wakati hamna akili,kuna wakati anakuwa na haiba nzuri,kuna wakati anakuwa kama mwehu,kuna wakati anakuwa na mawazo mazuri,kuna wakati mawazo yake ni mabaya tu. mtu wa hivi hata maisha yake huwa ni ya kuanguka na kusimama
1 samwel 16:23
Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi alipokishika kinubi na kukipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
huu ni mfano wa Mtu ambaye nafsi yake hushambuliwa na mapepo kutokea kwa nje,mara nyingi mtu huyu anaweza akawa ameokoka na kwa sababu hiyo mapepo hayawezi kukaa ndani yake hivyo roho chafu huja na kuondoka,mfano mtu anaweza akawa ni mgonjwa akiwa nyumbani lakini akifika kanisani anakuwa mzima wa afya.

3.      MAPEPO YALIYOSHIKISHWA NA NAFSI YA MTU.
kuna watu wengine nafsi zao huwa zinakuwa zimeshikishwa na nafsi nyingine,utaona mfano katika maandiko haya
1samweli 18:1
Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. 3Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. 4Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
Nafsi(roho) ya yonathani iliambatana na ya daudi,maana yake ni kuwa nafsi ya daudi na ya yonathani zilifungaanishwa ndani ya agano la upendo,hii ndio sababu unaona kuna wakati yonathani alikuwa akimgeuka hata baba yake kwa kushirikisha taarifa za siri kwa Daudi
kuna mapepo ambayo yanaweza kufungwanisha na nafsi ya Mtu,mtu ambaye nafsi yake imefunganishwa na mapepo,wakati mwingine hawezi kuwa na maamuzi ya kwake mwenyewe,hawezi kujitawala,na siri zake za ndani hutambulikana na mapepo na hivyo kujikuta njia zake za mafanikio zikijulika na kuzuiliwa.
wakati mwingine unaweza ukawa umefungamanishwa kiagano na nafsi ya mtu ambaye anamapepo,hivyo hata kama wewe huna mapepo unaweza ukajikuta unaambukizwa roho za rafiki yako aliye na mapepo maandiko yanasema.
amosi 3:3
Je! Watu wawili wanaweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?


NJIA AMBAZO MAPEPO HUZITUMIA KUJIPENYEZA KATIKA NAFSI YAKO.
1.      KUPITIA URAFIKI
1samwel 18:1
 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. 4Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
mtu anapofika katika eneo hili la urafiki,kuna mategemeo ya aina mbili,kwanba urafiki huu unaweza kumpa faida au kuharibu kabisa maisha yake,kwa sababu nafsi zinapoungana kupitia upendo zinafika katika kiwango cha kufanana,hii ni kwa sababu kuna vitu ndani ya nafsi vinahama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,hii ndio sababu maandiko yanasema.
2cor 6:14
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?Beliari maana yake ni, Ufisadi. Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
Biblia inasema msifungiwe nira na wasio amini,hii ni kwa sababu unapojenga urafiki wa upendo pamoja na mtu asiyeamini,inapelekea kufungwa pamoja kinafsi na hivyo kushirikiana viungo vya nafsi(tabia),unapokuwa na marafiki wengi wa kidunia si ajabu maisha yako yakaanza kurudi nyuma kiroho kwa sababu ya impact ya nafsi zao kwako.
2.      KUPITIA TENDO LA NDOA
tendo la ndoa huunganisha nafsi mbili kuwa moja maana yake ni kuwa kama mwanaumea ndani yake kulikuwa na mapepo ya aina Fulani na mwanamke alikuwa na mapepo au roho za aina Fulani wanapokutana kimwili huunganisha nafsi zao/mapepo yao na kuyafanya kuwa na nguvu ya kutawala maisha yao, kama ni Baraka hivyo hivyo huunganishwa
1cor 6:16
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
Unaona yeye alalaye na kahaba ameunganishwa naye,unapolala na mwanamke au mwanaume nafsi zenu zinaungana,na zinapoungana mtaanza kushare(kushirikishana) tabia zenu,Baraka zenu,laana zenu n.k na huu ndio mlango mkuu wa mapepo hasa kwa vijana. wengi hatima zao huharibiwa kwa namna hii,wanapolala na wanawake/wanaume wenye mapepo.
Mithali 6:31
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
Wala fedheha yake haitafutika.


unaona hapo mwanzo nilisema mapepo yanapokaa ndani ya nafsi ya mtu huharibu akili yake,na unaona maandiko yanasema alalaye na mwanamke(asiye wake) hana akili kabisa,hii ni kwa sababu ukilala na mwanamke ambaye ni kahaba yale mapepo huingia katika nafsi yako kupitia muunganiko wenu na kukukontrol kila kitu ndani ya nafsi yako na kuharibu kabisa mfumo wako wa kufikiri.
3.      KUPITIA VITU UNAVYOVIPENDA KUANGALIA AU KUSIKIA
Uaweza ukawa unapenda aina Fulani ya vitu,labda miziki ya kidunia,au picha za ngono,au filamu za aina mbalimbali,kumbuka hapo mwanzo nilikuambia ya Kuwa kazi ya moyo ni kupokea na kuhifadhi kila kitu kinachopita katika milango yako ya fahamu na kisha kukitoa nje,hii ndio sababu maandiko yanasema ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya.
sasa kama unasikiliza nyimbo ambazo ndani yake zimefungamanishwa na mapepo,au unaangalia filamu ambazo ndani yake zimefungamanishwa na mapepo,huingia ndani ya moyo wako na kuharibu kabisa mfumo wa nafsi yako.
katika kurasa za mwanzo niliandika ya kuwa wakati mwingine mapepo huingia ndani ya mtu kupitia kuona hii ndio sababu ayubu aliweka agano na macho yake.
zaburi 119:37
Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa,
Unihuishe katika njia yako.

DALILI ZA MTU AMBAYE ANAFSI YAKE IMEVAMIWA NA MAPEPO
1.      kupoteza kumbukumbu mara kwa mara
2.      kukosa uwezo mzuri wa kufikiri
3.      kuwa na mawazo mabaya mfano,mwawazo ya kiuasherati,kujiua,n.k
4.      kuinuka na kuanguka anguka katika wokovu na maisha
5.      kuwa na ndoto za kutisha mara kwa mara
6.      ukichaaa,uwazimu
7.      hasira na uchungu uliopitiliza
8.      hofu na mashaka ya mara kwa mara
9.      ulevi wa vitu mbalimbali (addiction)
10.  Tabia mbaya(bad Character)
11.  hali ya kukata tama haraka

inawezekana wewe ni muhanga wa hayo ambayo nimeyaonesha hapo juu,inawezekana upo katika eneo moja wapo.habari njema ni kuwa Unaweza kufunguliwa kabisa katika hayo maeneo tafadhali fuata Maelezo yaliyopo hapo chini.
maelekezo ya kinabii: chukua mafuta ya ukombozi kisha paka katika kichwa chako pamoja na katika moyo wake(eneo la nje kifuani) halafu anza kuomba maombi haya.
1.      Baba katika Jina la Yesu ninaomba Toba na msamaha juu ya kila jambo ambalo nimelifanya kwa kujua au kutokujua ambalo limeruhusu mapepo kupata uhalali wa kuishambulia au kukaa katika nafsi yangu.
2.      katika damu ya yesu ya thamani ninajifungua kutoka katika vifungo vyote vya nafsi yangu nilivyojifunga mwenyewe au ninilvyofungiwa na mapepo kwa kujua au kutokujua
3.      Kwa moto wa roho mtakatifu uteketeze kila mapepo yaliyokaa ndani ya moyo wangu,ndani ya akili zangu na ndani ya utu wangu katika jina la Yesu
4.      kila aina za roho zilizofunganishwa na nafsi yangu kutoka kuzimu ziharibiwe sasa kwamoto wa Roho mtakatifu katika jina la Yesu
5.      kila ndoto ambazo ni milango ya kipepo katika maisha yangu zihribiwe kabisa kwa jina la Yesu
6.      Ninarejesha nafsi yangu na sehemu zake katika ukamilifu wake katika jina la Yesu
7.      Damu ya yesu inene mema katika nafsi yangu katika Jina la Yesu
8.      ka damu ya yesu najipatanisha nafsi yangu na nafsi ya Mungu leo katika jina la Yesu.
Asante Yesu niko huru.

NB: Fika kanisani kwetu uonane na Nabii ili akupe maelekezo zaidi na kukuombea.



















KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA MADENI
2 falme 4:-5
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemdai amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta. Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache. 4Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.
Madeni ni roho sio kitu cha kawaida cha kuzoeleka, Biblia inasema  “ mdaiwa ni mtumwa wa anayedai”. Hii inamaana mtu anayekudai anaweza kukutumikisha anavyotaka, atakuwekea masharti anayoyataka yeye na utayafuta sababu uko chini ya deni. Anayekudai atakuwekea hata kiwango cha ukomo cha amani yako, Hii ndiyo sababu unapokutana na mtu anayekudai moyo wako unakosa amani.
Wapo wengi wamehama makanisa Kwa sababu ya kudaiwa. unajisikiaje unapokaa ikaribu na mtu anayekudai wakati wa kumwabudu Mungu kanisani?. Hii ndiyo sababu Mungu anasema Kumb 28 “utakopesha wala hutakopa”.
Sio watu wengi hutazama madeni kama roho, ndiyo sababu ni rahisi kunaswa katika mkono wa madeni.  Roho ya madeni haichagui mtu wa kumvaa na kumwendesha, haijalishi ni mtu mkubwa au mdogo, maskini au tajiri unapovamiwa na roho hii unakuwa mtumwa. Kuna watu ambao hawawezi kuishi bila kudaiwa, hata kama hawapendi kwasababu hii ni roho, itahakikisha baada ya kupata fedha unatumia haraka ili ukope tena, itahakikisha ukishalipa deni unakuwa na kiu ya kukopa tena.
Sasa maandiko hapo juu ya  utaona kuna  mtu aliitwa Elisha na alikutana na mmoja wa wake za manabii ambaye mume wake alifariki. Mama huyu alikuwa anadaiwa katika namna ambayo kama asingeweza kulipa watoto wake wangishia utumwani. Ndipo alipokutana na Elisha nabii ambaye aliachilia Neema ya utele iliyoshinda roho ya madeni. Hii inatudhihirishia ya kuwa mtu anaweza kutoka katika roho ya madeni kwa Neema ya Mungu inayoleta utele. Habari njema ni kuwa leo roho ya madeni itakomeshwa kabisa kwenye maisha yako katika jina la Yesu Kristo.
maelekezo ya kinabii ya I
Chukua Mafuta ya Upako ( Anointing Oil) kisha jipake kichwani kwako huku ukiomba maombi haya;(isaya 10:27)
1.      Baba katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba kwa damu yako kufutika kwa kila deni katika maisha yangu.
2.      kila nira na mzigo wa Madeni katika maisha yangu uharibiwe katika Jina la Yesu.
3.      Ninakemea na kuharibu kila roho ya madeni katika maisha yangu na watoto wangu, ninaiamuru iniachie kwa Jina la Yesu Kristo. (sema niachie kwa Jina la Yesu kwa sauti mara 7).
Maelekezo ya kinabii  II
Chukua kitu chochote kinachowakilisha chanzo chako cha kipato kisha anza kuomba maombi haya
1.      Kwa Jina la Yesu Kristo, Imeandikwa nimewekewa mlango wazi mbele yangu wala hakuna awezaye kuufunga. Hivyo kila mlango wa kipato uliofungwa au kuminywa naamuru ufunguke katika Jina la Yesu Kristo.

2.      Ninaamuru Baraka ya Utele kuja juu yangu na familia yangu kwa Jina la Yesu Kristo.
3.      Ninakataa kukopa, bali nitakopesha katika Jina la Yesu Kristo.


N.B Baada ya maombi haya Mungu amefungua milango yako, Hivyo hakikisha unafanya yafuatayo
·         Fedha inayokuja mkononi mwako tumia kulipa madeni.
·         Hakikisha kama unafanya kazi/ biashara unatoa fungu la kumi na dhabihu kwa BWANA ili apate kukuzidisha. kumb 8:18, malaki 3:10

            ------------ASANTE YESU MKO HURU----------


hakikisha unaendelea kufanya maombi ya ukombozi mara kwa mara,na kuanzia katika kurasa zinazofuata nimekuwekea maombi mengine ya ukombozi ili yakusaidie unapoendelea kuomba kwajili ya maisha yako.








MAOMBI YA UKOMBOZI.
1. Ninarudisha mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/mababa, katika Jina la Yesu.
2. Nina zilaani roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano katika maisha yangu na naziamuru kuniachia kwa Jina la Yesu[ Sema mara 3 na anza kusema hivi,”niachie kwa jina la Yesu
3. Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo, ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu
4. Kila aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa, katika jina la Yesu, nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5. Ee Bwana Yesu,shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu,iliyoandaliwa kwa ajili yangu, katika jina la Yesu
6. Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho, katika jina la Yesu
7. Upanga wa moto, na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi, katika jina la Yesu
8. Ee Bwana, nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu au anataka kufunga na nafsi yangu, katika jina la Yesu.
9. Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu, nina kungo’a katika jina la Yesu.
10. Baba nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu yangu lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.
11. Agano lolote la siri ambalo ni la uovu, ninakuvunja katika jina la Yesu
12. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote
13. [Imba wimbo huu kama unaweza, kama huwezi usilazimshe: Kuna nguvu ya ajabu, damuni mwa Yesu ]
14. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu
15. Ee Bwana, badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka
16. Kila nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu, ninakuamuru kurudi moja kwa moja, kwa mtumaji katika jina la Yesu.
17. Ee Bwana Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika maisha yangu, kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.
18. Nina jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na adui,katika jina la Yesu.
19. Nina jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina la Yesu.
20. Ee Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na uharibu/ulikate kila pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.
21. Nina ipitisha Damu ya Yesu, katika mifumo yote ya mwili wangu [mfumo wa damu, wa fahamu, wa chakula, wa upumuaji, wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote ya urithi wa vitu viovu katika jina la Yesu.
22. Damu ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu [Figo, moyo, mapafu, macho, masikio, n.k] katika jina la Yesu
23. Nina vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina la Yesu.
24. Nina jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika jina la Yesu
25. Nina tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha yangu, katika jina la Yesu
26. Mapepo, majini, mizimu na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na mpararaizi[mpooze] sasa katika jina la Yesu.
27. Shambulio lolote lilopangwa juu ya familia yangu, ninalibatilisha kwa ajili yangu katika jina la Yesu
28. Nina vunja matoke mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu, lilipachikwa kwenye nafsi yangu katika jina la Yesu
29. Nina batilisha laana zote, mikosi, majanga, ajali, maradhi yote yaliyoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
30. Muombe Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya kutotii neon lake[kumb 28:]
31. Pepo lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi, toka, katika jina la Yesu
32. Laana zote katika maisha yangu, badilika na kuwa Baraka, katika jina la Yesu
33. Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa hapo chini, sema kwa kumaanisha “vunjika, vunjika, vunjika” katika jina la Yesu. Nina jitenganisha na nyinyi katika jina la Yesu.
• Laana zote za udhaifu wa kiakili na kimwili
• Laana zote za kushidwa katika kila ninalofanya
• Laana zote za umaskini
• Laana zote za kuvunjika kwa familia
• Laana zote za kuonewa na kudharauliwa
• Laana zote za Uharibifu wa mtu binafsi,kama vile kujinyonga n.k
• Laana zote za magonjwa sugu
• Laana zote za kishirikina
• Laana zote za kuharibikiwa mambo ya uzazi na viungo vya uzazi
• Laana zote za kufanya kazi kwa bidii pasipo kuiona faida
• Laana zote za kulowea mambo ya uovu kama vile zinaa, pombe, sigara n.k
34. Jitamkie maneno ya Baraka wewe mwenyewe, kwa mfano kwa kusema “hakutakuwa na umaskini tena, magonjwa tena n.k katika maisha yangu katika jina la Yesu.
35. Nina jifungua na kujitenganisha na vifungo vya madhabahu zote za giza katika jina la Yesu.Sema mara kadhaa ukifuatiwa na maneno yafuatayo “nina jitenganisha” katika jina la Yesu.Tumia muda kidogo kwenye hilo.
36. Nina tapika sumu zote za mashetani nilizozimeza katika jina la Yesu.
37.[Weka mikono yako juu ya kichwa chako] Nina vunja kila mamlaka za giza katika maisha yangu, katika jina la Yesu.Rudia “nina vunja katika jina la Yesu.
38. Taja mambo yafuatayo kwa mamlaka na sema “vunjika kwa jina la Yesu.
• Mamlaka zote za mizimu na miungu ya familia, ukoo, na kabila
• Mamlaka zote za roho za kichawi zilzopo ndani ya familia, ukoo, kabila
• Mamalaka zote zilizoshika rimoti za kudhibiti familia, ukoo, kabila
• Mamlaka zote ovu ndani ya Familia, ukoo, kabila nk
39. Kila mmiliki wa mzigo niliobebeshwa beba mzigo wako katika jina la Yesu[Mzigo unaweza kuwa ugonjwa,mikosi wabebeshe wamilki]
40. Nina zipoodhesha/nina zipararaizi madhabahu zote za giza katika jina la Yesu
41. Nina zilaani madhabahu zote za uovu zilizoelekezwa zidi yangu katika jina la Yesu
42. Nina agiza nyundo ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi,iponde kila madhabahu ya giza zilizoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
43. Ee Bwana tuma moto wako na uteketeze madhabahu zote za giza zinazoinuka dhidi ya maisha yangu,
44. Makuhani wote wa madhabahu zote za giza wanaocheza na maisha yangu,wakutane na upanga wa roho mtakatifu. Katika jina la Yesu.
45. Mkono wowote unaotaka kunikamata na kuniteka kwa ajili ya Maombi haya ninayoomba kauka katika jina la Yesu.
46. Nina waamuru makuhani wa madhabahu za giza kunyweni damu wenyewe katika jina la Yesu
47. Nina rudisha urithi wangu ulioibiwa na madhabahu za giza katika jina la Yesu.
48. Ninafuta/ninaliondoa jina langu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
49. [Weka mkono wako mmoja kifuani] Ninaziondoa Baraka zangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
50. [Weka mkono mmoja kifuani na mwingine kichwani] Ninaondoa kitu chochote kile kinachoniwakilisha mimi [kama vile nguo] kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu.
51. [Taja kiungo chochote katika mwili wako ambacho akifanyi kazi ipasavyo au kama ni mwili wote taja mwili] na useme maneno yafuatayo “nina kuondoa kwenye madhabahu za giza” katika jina la Yesu. Tamka hivyo mara saba.
52. Nina jitenganisha kutoka kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza katika jina la Yesu
53. Damu ya Yesu na unene kwa ajili yangu dhidi ya maagano yote na nguvu za giza
54. Nina tamka Uharibifu dhidi ya roho chafu zote katika maisha yangu.Katika Jina la Yesu.
55. Nina jitenganisha na laana zote za maagano katika jina la Yesu
56. Nina jitenganisha mimi na familia yangu kutoka katika kila agano la damu katika jina la Yesu.
57. Ninajitenganisha na kila agano la damu la kurithi katika jina la Yesu.
58. Nina iondoa damu yangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
59. Nina iondoa damu yangu kutoka kwenye benki za damu kwenye ulimwengu wa giza katika jina la Yesu
60. Nina vunja kila agano la damu la kutokukusudia kwa jina la Yesu
61.Ee bwana, damu ya mnyama yeyote iliyomwagika kwa niaba yangu, Naipoteze nguvu ya agano sasa, kwa jina la Yesu
62. Kila tone la damu linalotamka mabaya dhidi yangu, na ikae kimya sasa, kwa damu ya Yesu
63. Ninajifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila agano la damu la kifamila, kiukoo, kabila katika jina la Yesu.
64. Nina jitenganisha na kila agano la damu nililoingia kwa kujua au kutojua kwa jina la Yesu
65. Ee Bwana kila agano la damuna nguvu za giza lipoteze nguvu na uhalali wake juu yangu katika jina la Yesu.
66. Damu ya agano jipya la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo, naiikemee damu ya agano na nguvu za giza ilijipanga kinyume name. Kwa jina la Yesu
67. Nimepewa mamlaka ya kubatilisha haki zote zilizopo kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza .kwa jina la Yesu.
68.Agano lolote la damu na nguvu za giza lililofungwa kwenye kiungo chochote kwenye mwili wangu, nalivunjike sasa.Kwa jina la Yesu
69. Ninapokea vitu vyote vilivyoibiwa au kuchukuliwa na adui kupitia maagano na nguvu za giza. Kwa jina la Yesu.

70. Nina vunja agano lolote la damu na nguvu za giza kwenye damu yangu . Kwa jina la Yesu



1 comment:

  1. Unamafundisho mazuri mtumishi wa Mungu, ubarikiwe sana. By Mch. Mathew Dr. of Theology and Community Development.

    ReplyDelete