MUNGU WA MAAGANO

 


MUNGU WA MAAGANO

Yer 33:19-22 SUV

*Neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, BWANA asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake, ndipo agano langu nililolifanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi; tena agano langu nililofanya na Walawi makuhani, wahudumu wangu, laweza kuvunjika. Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi wanaonihudumia*

 

Dan 9:4 

 

*Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake*

 

*Watu wengi wanashindwa kutembea na Mungu kwa muda mrefu kwa sababu hawajamwelewa mungu namna anavyo fanya kazi zake,na moja kati ya vipengere vya muhimu katika kutembea na Mungu katika Maisha ni kutembea na Mungu kiagano*

 

Hakuna jambo litakalo kupa uhakika wa Maisha yako ya sasa na ya baadae kama kuwa na agano na Mungu hii ni Muhimu sana

 

Tunaposoma neno la mungu katika waebrania 11,tunawaona mashujaa wa Imani wakitajwa,lakini utaona asilimia 99 ya hawa wanaoitwa mashujaa wa imani ushujaa wao ulitokana na kutembea na mungu kiagano.

Ni ukweli usiopingika ya kuwa zipo ahadi nyingi zinazogusa kila kona ya Maisha ya mtu katika Biblia,Mungu ameahidi uponya,ulinzi,uzao,mafanikio,msaada wa haraka n.k ,lakini si watu wengi wanazifikia ahadi hizo,unaweza ukazijua ahadi zote za Mungu lakini utimilifu wake ni matokeo ya Agano.

 

Mungu si Mungu wa Ahadi ni Mungu wa Maagano,yeye Hushika maagano na Rehema

Dan 9:4 

*Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake*

 

Hii ndio siri iliyofichwa tangu zamani za kale,ni hekima iliyofichwa na ni maajabu ya ufalme yanayoleta uhakika wa Maisha ya sasa nay a Baadae.

 

Agano na Mungu ni nini?

Agano na Mungu ni makubaliano yako wewe na Mungu yanayo Ma Mungu uhalali wa kukusaidia katika maeneo Fulani ya kimaisha,ni Mkataba kati ya pande mbili unaohusisha utekelezaji wa majukumu kwa faida ya wote,maana yake Mungu atakupa faida na wewe ni lazima ufanye jambo la faida kwake,ni makubaliano ya kutembea Pamoja katika eneo Fulani.

 

Amo 3:3 

*Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana*?

 

Hebu tuangalie mfano wa agano la Mung una Ibrahimu

 

 

Mwa 17:1-25 SUV

*Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao. Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako. Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele. Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu. Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake. Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako. Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana*

 

Katika mfano huu wa andiko hapo juu utaona Kuna vipengere vinne ambavyo vinakamilisha agano

1.     *Mungu ndiye anayekupa agano*

 

Tofauti na watu wengi wanavyofahamu ya kuwa ni wao wanaweka agano na Mungu,kibiblia ni Mungu ndiye anayekuba agano,na Mungu akikupa agano agano lake ni la Milele.

 

Mungu alishamaliza kuandika maagano yaani vipengere vya makubaliano katika maeneo mbalimbali na nini atakachofanya utakapokubali kuingia nae agano,vipengere hivi ndio tunaviita ahadi,hii ndio sababu haiwezi kukusaidia sana wewe kushika vipengere vya agano kabla ya kuingia agano na Mungu

 

Mwa 17:1-25 SUV

*Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana*

 

Unapoona kuna haja ya kutembea na Mungu katika eneo Fulani la kimaisha,anagalia vipengere vya neno la Mungu vinavyozungumzia changamoto unayoipitia kisha ingia katika agano na Mungu

 

2.     *Mungu anakubadilisha jina na kukupa utambulisho wako halisi*

 

Mara nyingi majina yetu ndiyo yanayotutambulisha kwa watu,ni majina tumepewa na wazazi wetu,lakini lipo jina linalobeba utambulisho wako halisi na jina hilo ni jina la kiagano,ni jina ambalo Mbingu inakutambua nalo.

Unapotembea na Mungu kiagano hauwezi kubabe utambulisho ule ule ambao ulikuwa nao kabla ya agano hii ni kwa sababu jina la Mtu hubeba Nguvu zake,mipaka yake na uwezo wake,pia hubeba utambulisho wake na tabia zake

 

Hii ndio sababu Mungu akitaka kutembea na wewe atakupa utambulisho mpya ambao utaendana na agano analokupa,hii inamaana kuwa atakupa nguvu mpya,akili mpya ,tabia mpya n.k

 

Mwanzo 17

* Mungu akamwambia, akasema, Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi*

 

Si ibrahimu peke yake ambaye alibadilishwa jina,ipo mifano ya mashujaa wengine pia,unasoma

 

Mwa 32:28 

*Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda*

 

Yn 1:42 SUV

*Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa *(tafsiri yake Petro, au Jiwe).

Japokuwa si wote ambao Mungu huwapa agano hubadilishwa majina,lakini hii huwa ni hatua muhimu sana kuelekea mabadiliko katika kiwango cha kiagano.

 

3.     *Ahadi za Agano*

Ahadi za agano ni matokeo ya uaminifu wako kwa Mungu juu ya vipengere vya kiagano,kwa lugha rahisi tunaweza sema faida za kuingia agano na Mungu.

 

Mwanzo 17

“…Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao. Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa…”

 

unapoamua kujitoa kwa uaminifu juu ya agano lako na Mungu ndipo Mungu atakutimizia ahadi zake za kiagano.

 

4.     *Majukumu ya kiagano*

 

Hapa ndio wengi huwa tunafeli,wengi hutelekeza majukumu katika nyakati za kwanza na baada ya muda hujisahau au kuacha kabisa.

Hii ndio sababu mwanadamu hawezi kubaki wa kuaminiwa katika eneo la maagano,ni Mungu peke yake hubaki wa kuaminiwa

 

Malaki 3:6 SRUV

*Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo*

 

Ni Gharama katika kutekeleza majukumu ya kiagano,na wakati mwingine unaweza usipende kile ambacho Mungu anakwambia ufanye lakini kama unataka kufurahia mabadiliko ni lazima ufanye.

Wakati nimeingia kwenye agano na Mungu la utumishi kuna mamboa ambayo niliambiwa sitakiwi kufanya,mambo hayo si dhambi kwa mtu wa kawaida kufanya lakini kwangu ni mwiko.

 

Ibrahimu aliambiwa mambo yafuatayo.

i.                    Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.

 

ii.                  Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako. Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.

 

Hasara za kutokushika makubaliano.

 

i.                    Kutengwa mbali na watu wako

…… Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu….

 

ii.                  Kuharibiwa kwa kazi za mikono yako

Muh 5:6

Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako? 

 

 

iii.                Kutokufika kule ambako Mungu alitaka ufike

Hes 20:12 SUV

 

*BWANA akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa*

 

 

*Faida za Kuwa na Agano Na Mungu*

i.                    Kuwa na uhakika wa Baadae yako

ii.                  Kutembea na mungu katika eneo ambalo umeweka nae agano,kama ni katika Biashara,kazi au ndoa

iii.                Agano linakupa Ulinzi wa Kiungu kwenye eneo la kiagano

iv.                Agano linahakikisha ahadi za Mungu zinatimia sawa sawa na Makubaliano Yenu

v.                  Agano linakupa kibali

vi.                Ni uhakika ya kuwa Mungu yupo katika eneo lako

NB; *Unaweza kuingia na Mungu katika agano kutegemeana na uhitaji wa Maisha yako*

 

Imeandaliwa na

*Rabbi and Prophet Calvin Raphason*

Spirit of life Ministries

Mawasiliano *0757370010/0797680106/0773700106*

 

Comments