UKOMBOZI WA ARDHI (Mwl Melechzedech Shalua)


UKOMBOZI WA ARDHI (Mwl Melechzedech Shalua)
SEMINA YA NENO LA MUNGU YA SIKU TATU (TAR 05-07/02/2016) KATIKA UKUMBI WA KWIDEKO – NGUDU KWIMBA. IMEANDALIWA NA NURU FELLOWSHIP NA UZIMA WA MILELE INTERNATIONAL MINISTRIES KWA KUSHIRIKIANA NA HUDUMA YA MANA MKOA WA MWANZA.

SIKU YA TATU (TAR 07/02/2016)
UKOMBOZI WA ARDHI ……….. Inaendelea – Mwl Melechzedech Shalua

Ø  Kwakweli ardhi inatoa maamuzi juu ya watu wanaokaa juu yake kwa kutegemea imekabidhiwa kwa Mungu yupi.
Ardhi inaweza kuolewa na kuzaa matunda kutegemea na Mungu aliyeioa, Isaya 62:4-5“4 Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako itaolewa. 5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.”

Ø  Ardhi haiwezi kuzaa pasipo kuolewa na kuzaa huko kunategemea na Mungu/mungu aliyeioa ardhi hiyo.

Uzao wa ardhi unaweza kubarikiwa na pia unaweza kulaaniwa, Kumb 28:4,18“4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.”

Ø  Ardhi inaweza kuwa haizai kutokana na laana. Ukiisemesha tu ardhi inaweza kuzaa kwaajili yako hatakama haizai kwaajili ya wengine
Asili ya kila kitu chenye uhai ni ardhi, Mwanzo 2:4-19
-          Bwana Mungu Akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi
-          Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti……….
-          Bwana Mungu akamfanyizi katika ardhi kila myama…..

Ø  Nchi/ardhi inaweza kuwatapika wenyeji na kuwatoa,
 Walawi 18:24-25“24 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa.”

Ø Nchi ikiwa najisi kwasababu ya wanadamu kuifanya iwe najisi, Mungu anaachilia adahbu juu ya hiyo nchi na nchi inaanza kuzaa mapooza

2Wafalme 2:19-22“19 Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. 20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. 21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. 22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.”
Ndio maana Mungu anasema ataiponya nchi ikiwa watu wake walioitwa kwa jina lake watajinyenyekesha na kuomba, hii inamaana kuwa ardhi inaweza kuwa na ugonjwa na ndio maana Mungui anaweza kuiponya kwani hauwezi kuponya kisichoumwa
Damu ikimwagika kwenye ardhi, ardhi haiwezi kunena mema

2Samwel 21:1-4“1 Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni. 2 Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi yake kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;) 3 basi Daudi akawaambia hao Wagibeoni, Niwatendee nini? Na kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa Bwana? 4 Na hao Wagibeoni wakamwambia, Si jambo la fedha wala dhahabu lililo kati ya sisi na Sauli, au nyumba yake; wala si juu yetu kumwua mtu ye yote katika Israeli. Akasema Mtakayoyanena, ndiyo nitakayowatendea ninyi.”

Ø  Ardhi inao uwezo wa kusikia, kutunza kile ilichosikia na kutekeleza kile ilichosemeshwa
Kumb 30:19-2019 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; 20 kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.”

Musa anapoongea na wana wa Israel anafanya mbingu na nchi kuwa shahidi ili ikumbukwe daima

Kumb 31:14-30“24 Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya torati hii katika chuo, hata yakaisha, 25 ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la agano la Bwana akawaambia, 26 Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako. 27 Kwa kuwa uasi wako naujua, na shingo yako ngumu; angalieni, mimi nikali hai pamoja nanyi leo, mmekuwa waasi juu ya Bwana; siuze nitakapokwisha kufa! 28 Nikutanishieni wazee wote wa kabila zenu, na maakida yenu, ili niseme maneno haya masikioni mwao, na kuwashuhudizia mbingu na nchi juu yao. 29 Kwa sababu najua baada ya kufa kwangu mtajiharibu kabisa, na kukengeuka katika njia niliyowaamuru; nayo mabaya yatawapata siku za mwisho, kwa vile mtakavyofanya maovu machoni pa Bwana kumtia kasirani kwa kazi ya mikono yenu. 30 Musa akasema maneno ya wimbo huu masikioni mwa kusanyiko la wana wa Israeli hata yakaisha.”

Kumb 32:1“1 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu.”

Yeremia 22:29-30“29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. 30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.”

Ø  Unaweza kufanya eneo kwenye ardhi kuwa sehemu ya kukutana na Mungu wako
Madhabahu ya Munguu inajengwa na Yakobo katika ardhi ili pawe ukumbusho wa agano

Mwanzo 28:16-22“16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. 17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. 18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. 19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. 22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

Alama unayoiweka kwenye ardhi ni ukombusho wako na Mungu wako

Mwanzo 35:6-7“6 Basi Yakobo akafika Luzu, ulio katika nchi ya Kanaani, ndio Betheli, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. 7 Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.”

Ø  Ardhi inao uwezo wa kufurahi na kuwafurahisha wanaokaa juu yake kwasababu ya toba iliyofanywa ili kuirejesha ardhi kwa Mungu

Ardhi inayoomboleza inanyima Baraka kwa watoto wa Mungu, Yoeli 1:10“10 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.”

Baada ya kwenda mbele za Mungu kwa toba Mungu anatoa Baraka juu ya ardhi, ardhi inafurahi na kutoa matunda

Yoeli 2:21“Ee nchi, usiogope; furahi na kushangilia; kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu.”

Unapoomba toba na kubomoa madhabahu za giza na kubariki ardhi nayo ardhi inafurahi

Yeremia 51:48-49“48 Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjilia kutoka kaskazini, asema Bwana. 49 Kama vile Babeli alivyowaangusha watu wa Israeli waliouawa, ndivyo watakavyoanguka katika Babeli watu wa nchi yake nzima waliouawa.”

Ø  Ardhi iano uwezo wa kumuondoa mtu na kumlinda mtu aliye juu yake. Haijalishi kama unajua au haujui kawaida ya miungu/Mungu wa mahali unapokaa, kama ukikosea utashambuliwa/utapigwa na Mungu/miungu

2Falme 17:24-28“24 Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake. 25 Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha Bwana; kwa hiyo Bwana akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao. 26 Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi. 27 Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi. 28 Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha Bwana.”

Ø  Mapepo yanaweza kumilikishwa ardhi na yakadai kisheria kuwa na uhalali wa kuwepo mahali pale walipomilikishwa

Marko 5:1-17“1 Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. 2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. 11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. 12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. 13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. 14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea. 15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. 16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. 17 Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao.”

-          - Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi/ardhi ile……..Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao……….


JINSI YA KUOMBA/KUKOMBOA ARDHI

ü  Anza na toba na kuomba utakaso wa Damu ya Yesu ili Damu iweze kufuta uhalali wa umiliki wa miungu mingine ili usishambuliwe
ü  Tumia vifungu vya Biblia kumnyang’anya na kumuondoa shetani katika ardhi. Tumia sheria ya kimbingu kumhukumu shetani
ü  Tumia nyayo katika kumiliki na kutawala (Kwanini nyayo na sio viatu?)

a.       Kumb 11:22-24“22 Kwa kuwa kwamba mtayashika kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye; 23 ndipo Bwana atakapowafukuza mataifa haya yote mbele yenu, nanyi mtamiliki mataifa makubwa yenye nguvu kuwapita ninyi. 24 Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.”

b.      Yoshua 3:14-16“14 Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, 15 basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno), 16 ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.”

c.       Yoshua 1:3“Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.”

No comments:

Post a Comment